Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 16 January 2014

VOGTS, WOLFGANG WAIBUKIA KAMBI YA YANGA

Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani ambao kwa sasa ni makocha wa timu ya Taifa ya Azerbeijan Berti Vogts na msaidizi wake Wolfgang leo jioni kabla ya mazoezi waliibuka katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach na kuongea kidogo na makocha wa Young Africans Hans na Mkwasa masuala ya kiufundi kisha kuagana nao na kuwaacha waendelee na progam yao ya mazoezi.
Vogts amabaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Ujerumani kwa miaka nane (1990-1998) na kufanikiwa kushinda kombe la Ulaya mwaka 1996, na kufika hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia mwaka 1998 alikuwa ameambatana na kocha wake msaidizi Wolfagang .
Kocha mpya wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum leo ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side baada ya jana kuiongoza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.

Mkwasa na Wolfagang

Hans ambaye amejiunga na Young Africans wiki hii akichukua nafasi ya kocha mholanzi aliyeondoka Ernie Brandts amesema atajitahid kadri ya uwezo wake pamoja na wachezaji na benchi la ufundi kuona wanaisaidia timu kufika hatua nyingine mbele zaidi.
"Amesema hawezi kufanya jambo lolote peke yake bali kwa kushirikiana kwa pamoja atafanikiwa kwani katika mchezo wa jana timu yake iliweza kucheza soka la kujituma na kushirikiana mwanzo mwisho kitu ambacho ndio falsafa yake katika ufundishaji" alisema Hans.
Timu ilifanya mazoezi ya asubuhi leo saa 5 kamili kwa saa za Uturuki mpaka saa 6:30 kabla ya kupumzika na kurejea tena mazoezini jioni saa 11 kamili jioni mpaka saa 12:30 ambapo alikuwa akiwaelekeza wachezaji jinsi gani anapendelea wacheze kwa kufuata mfumo wake.




Kocha Msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa akiwa na Kocha Berti Vogts

No comments:

Post a Comment