Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday 15 January 2014

SIMBA SC KUCHEZA NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI


Simba SC itacheza mchezo wa kirafiki na Mtibwa Sugar ya Morogoro Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo unakuja siku chache baada ya timu hiyo kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, kufuatia kufungwa 1-0 na KCC ya Uganda Jumatatu wiki hii, Uwanja wa Amaan, Unguja. Aidha huo utakuwa mchezo wa kwanza Simba kucheza nyumbani, tangu imfunge mpinzani wake wa jadi, Yanga SC 3-1 kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 21, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment