Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday 3 November 2013

ANGETILE OSIAH MALABEJA ANG'OLEWA TFF, WAMBURA ANAKAIMU NAFASI YAKE



Na Mahmoud Zubeiry, Posta
KIKAO cha kwanza cha Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana chini ya Rais, Jamal Emil Malinzi kimemuengua Katibu Mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah Malabeja.
Rais Malinzi, alifungua kikao kwa ajenda ya kumuengua Angetile na Wajumbe wakaafiki, lakini wanamng'oa kistaarabu.
Angetile amepewa likizo ya hadi atakapomaliza Mkataba wake mwezi ujao na kwa sasa, aliyekuwa Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura Mgoyo atakatimu nafasi yake.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.

Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.

Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.

Jamal Malinzi

Rais, Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment