Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 4 March 2014

TFF KUWACHUKULIA HATUA ZAIDI WAWILI TWIGA STARS

Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.
Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.


Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.“TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza,” imesema taarifa ya TFF.
Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.
Wakati huo huo: Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA), Lina Mando amesema shirikisho lake kupitia Kamati ya Wanawake ya mpira wa miguu kwa wanawake, Linna Kessy wanatambua umuhimu wa siku ya wanawake duniani.
“Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani. Idadi ya wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Katika kusheherekea siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF /TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa miguu wanawake ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.
Walimu hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.
Ni matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake.

No comments:

Post a Comment