Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 4 March 2014

MARTESACKER NA ROSICKY WAONGEZA MIKATABA ARSENAL

NYOTA wawili wa Arsenal, Per Mertesacker na Tomas Rosicky wamekubali kusaini mikataba mipya ya kuendelea kupiga kazi Uwanja wa Emirates.
BIN ZUBEIRY inafahamu The Gunners imekuwa ikiwatongoza wachezaji hao kuongeza mikataba tangu Septemba mwaka jana - na sasa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imethibitisha wachezaji hao wanabaki.
Mertesacker ametweet picha akiwa kijana mdogo amevaa jezi ya Arsenal na kuandika maelezo: "Tangu nikiwa mdogo hadi sasa, najivunia kuwa gunner! Asante mashabiki kwaa sapoti yenu. Furaha kuongeza muda na @Arsenal.

Bado yupo sana; Beki Mjerumani Per Martersacker ameongeza Mkataba Arsenal hadi mwaka 2017

+9

Wanabaki: Rosicky na Mertesacker wameongeza mikataba yao Emirates
"Tuna furaha kwamba Mertesacker na Rosicky wamejifunga mustakabali wao katika klabu,"amesema kocha Arsene Wenger.
Kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, Rosicky amesaini Mkataba wa miezi 12 zaidi wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja na ataendelea kulipwa Pauni 80,000 kwa wiki.
Beki la kimataifa la Ujerumani, Mertesacker inafahamika amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu, utakaokwenda hadi mwaka 2017. Lakini yeye mkataba wake mpya ataongezewa mshahara kutoka Pauni 80,000 kwa wiki anazolipwa sasa.
+9
Mtutu mdogo: Per Mertesacker ametweet picha yake akiwa mdogo amevaa jezi ya Arsenal baada ya kukubali kusaini mkataba mpya

No comments:

Post a Comment