Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 8 March 2014

ZAMALEK YAPENYA TUNDU LA SINDANO, WAGANDA WAFANYA MADUDU KAMPALA BAADA YA KUANZA VIZURI MECHI YA KWANZA

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
ZAMALEK ya Misri imepenya kwenye tundu la sindano kuelekea Hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kulazimisha sare ya bila kufungana Angola usiku wa jana mbele ya wenyeji Kabuscorp katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza.
Zamalek inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Misri na Tottenham Hotspur ya England na klabu hiyo ya Cairo, Ahmed Hassan ‘Mido’ ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani na kutengeneza hofu ya kutolewa.

Wazembe hawa; KCC ilianza kwa sare ya 2-2 ugenini, lakini imefungwa 2-1 nyumbani leoKatika mechi za leo, KCC ya Uganda imeaga kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-3, ikifungwa 2-1 leo Kampala na Nkana FC ya Zambia baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza.
ASFA Yennenga ya Burkina Faso imeaga kwa kipigo cha jumla cha 5-0 kwa ES Setif ya Algeria baada ya sare ya 0-0 leo nyumbani, ikitoka kufungwa 5-0 Algiers wiki iliyopita na Primeiro de Agosto ya Angola imeaga kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-3 ikishinda 2-0 leo nyumbani baada ya kufungwa 4-1 na AC Leopards ya Kongo katika mchezo wa kwanza Brazzavile.
Liga Muculmana ya Msumbiji imetolewa pia kwa jumla ya mabao 7-0 na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini leo ikifungwa 3-0 nyumbani baada ya kufungwa 4-0 katika mchezo wa kwanza.
AS Real ya Mali iko nyumbani Bamako muda huu inamenyana na Enyimba ya Nigeria baada ya ushindi wa 2-1 ugenini katika mchezo wa kwanza na Raja Casablanca ya Morocco pia iko nyumbani Casablanca muda huu inamenyana na Horoya ya Guinea baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza ugenini.
Michuano hiyo itaendelea kesho, mabingwa watetezi Al-Ahly ya Misri wakijaribu kukipiku kipigo cha 1-0 kutoka Yanga SC ya Tanzania, Ahli Benghazi ya Libya ikiikaribisha Berekum Chelsea ya Ghana baada ya sare ya 1-1 ugenini, Esperance ya Tunisia ikiikaribisha Gor Mahia ya Kenya baada ya ushindi wa 3-2 Nairobi, Coton Sport ya Cameroon ikiikaribisha Flambeau de l’Est ya Burundi baada ya ushindi wa 1-0 Bujumbura, TP Mazembe ya DRC ikiikaribisha Astres Douala ya Cameroon baada ya sare ya 1-1 Douala, Sewe Sport ya Ivory Coast ikiikaribisha Barack Young Controllers ya Liberia baada ya sare ya 3-3 Monrovia.
CS Sfaxien ya Tunisia itakuwa mwenyeji wa Dedebit ya Ethiopia baada ya ushindi wa 2-1 Addis Ababa,
El Hilal Sudan itaikaribisha Stade Malien baada ya sare ya bila kufungana Mali na AS Vita Club ya DRC itaikaribisha Dynamos ya Zimbabwe baada ya sare ya bila kufungana Harare.

No comments:

Post a Comment