Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 3 March 2014

OKWI NA KIIZA TAYARI WAPO ZAMBIA NA THE CRANES, WATAONDOKEA HUKO KWENDA CAIRO

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
WASHAMBULIAJI Waganda wa klabu ya Yanga SC, Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza wamewasili jioni hii mjini Ndola, Zambia kujiunga na timu yao ya taifa, Uganda, The Cranes kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa Jumatano dhidi ya wenyeji Chipolopolo.
Okwi na Kiiza ambao waliichezea Yanga SC Jumamosi ikiifunga Al Ahly ya Misri bao 1-0 katika mchezo wa kwanza kuwania kutinga Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa, Dar ves Salaam waliondoka leo nchini.

Watu wa kazi; Okwi kulia akiwa na Kiiza, tayari wapo Zambia kuitumikia timu yao ya taifa ya UgandaKocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kutoka Ndola kwamba wachezaji hao wamefika salama na wataichezea The Cranes Jumatano kabla ya Alhamisi kwenda Cairo kuungana na klabu yao kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Al Ahly.
Kikosi cha Yanga SC kilichoingia kambini leo hoteli ya Bahari Beach kujiandaa na mchezo wa marudiano na Al Ahly, kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Alhamisi usiku kwenda Cairo.
Uongozi wa Yanga SC ulijaribu bila mafanikio kumshawishi Micho aliyewahi kuifundisha klabu hiyo mwaka 2007 awaache wachezaji hao waendelee na maandalizi ya pamoja na wenzao kwa ajili ya mechi na Ahly.
Lakini Micho amewaahidi Yanga SC atahakikisha yeye mwenyewe wachezaji wanaondoka mara tu baada ya mechi hiyo iliyo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimtaifa (FIFA).

No comments:

Post a Comment