
Kiungo wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' kushoto akiwatoka wachezaji wa JKT Oljoro ya Arusha jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba SC ilishinda 4-0.

Shujaa wa hat trick; Mrundi Amisi Tambwe kushoto jana alifunga mabao matatu peke yake

Mpishi wa mabao; Ramadhani Singano 'Messi'kulia jana alitoa pasi za mabao yote

Mtu wa kazi; Awadh Juma Issa kushoto jana alicheza vyema nafasi ya kiungo

Winga teleza; Haroub Chanongo kushoto jana aliwakimbiza sana pembeni mabeki wa Oljoro

Guu la kushoto upande wa kulia; Messi japokuwa anatumia mguu wa kushoto, lakini hucheza upande wa kulia

Kitu nyavuni; Tambwe kulia akiuangalia mpira aliopiga ukitinga nyavuni, huku kipa wa Oljoro na beki wake wakimsaidia kushuhudia bao la pili jana la Simba

Asante Mungu; Amisi Tambwe akiwa amesujudu baada ya kufunga

Kikosi cha Simba SC jana

Kikosi cha JKT Oloro jana
No comments:
Post a Comment