Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday, 20 December 2013

Hawa ndiyo mawaziri waliotenguliwa majukumu yao


Kufuatia majadiliano yanayoendelea Bungeni kuhusu ripoti iliyotolewa na kamati ya ardhi maliasili na utalii, Rais Jakaya Kikwete ametengua majukumu ya mawaziri wanne wa wizara za Maliasili na Utalii,Mambo ya Ndani,Ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa,pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia maamuzi hayo mawaziri wa Wizara hizo ambao ni Balozi Khamis Kagasheki waziri wa mali asili na utali ambae jna alikwisha kujiuzulu,Shamsi Vuai Nahodha waziri wa ulinzi na usalama,Emmanuel Nchimbi waziri wa mabo ya ndani na Mathayo David Mathayo waziri wa mifugo wameondolewa rasmi nyadhifa zao za uwaziri katika wizara hizo hadi uamuzi mwingine utakapotangazwa na Rais.

Uamuzi huu wa Ris Kikwete umetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja zilizotolewa na Wabunge.
KWA HABARI KAMA HIZI ZAIDI SOMA www.hakileo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment