Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 17 December 2013

SHIRIKISHO LA SOKA UGANDA LAANDIKA BARUA FIFA KUULIZIA UHALALI WA USAJILI WA OKWI YANGA.



Shirikisho la soka nchini Uganda limeandika barua kwenda FIFA likisaka ufafanuzi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyeuzwa kutoka SC Villa kwenda Yanga.

Siku ya jumatatu, Okwi alirirpotiwa kujiunga na mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Yanga kwa ada ya uhamisho wa $100,000 kwa mkataba wa miaka miwili, na huku huko nyuma FIFA ilimuidhinisha Okwi kujiunga kwa mkopo na klabu ya SC Villa akitokea klabu ya Tunisia Etoile du Sahel.

Okwi ameichezea SC Villa katika ligi kuu ya Uganda kwa kipindi cha takribani miezi miwili akiifungia timu hiyo mabao matatu.

“Tumeiandikia barua FIFA kwa sababu tunahitaji watueleze kama uhamisho huo ni sahihi," alisema CEO wa FUFA, Edgar Watson.

Lakini mkurugenzi wa SC Villa, Edgar Agaba, aliongea na mtandao wa mntfootball na kusema kwamba mchezaji huyo alijiunga na klabu ya Yanga akiwa mchezaji huru.

Wiki iliyopita shirikisho la soka Afrika kilisema kwamba Okwi na Godfrey Walusimbi hawakuwa na uhalali wa kucheza kwenye michuano ya 2014 Africa Nations Championships (CHAN) kwa sababu walikuwa na matatizo na vilabu vyao vya zamani Etoile du Sahel na Don Bosco (DR Congo).

Itakuwa jambo la kuvutia kuona namna Okwi, ambaye alizuiliwa kucheza CHAN, akiruhusiwa kujiunga na klabu ya Yanga na huku akiripotiwa kuwa na matatizo na klabu ya Etoile du Sahel.hili.” alisema Watson.

No comments:

Post a Comment