Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 21 December 2013

BAADA YA KIPIGO CHA 3-1 YANGA KUITISHA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KESHO, MINZORO AWAPONDA KINA KAVUMBAGU



Wakati uongozi wa klabu ya Yanga
umeitisha mkutano na waandishi wa
habari kesho (Desemba 22), kocha
msaidizi wa mabingwa hao, Fred
Felix Minziro amesema wakati wa
kupanga timu kwa mazoea sasa
umekwisha na wachezaji wanaocheza
soka la mdomoni hawana nafasi
katika timu yao.
Minziro alisema hayo wakati
akizungumzia timu yake huku
akiponda kikosi cha kwanza na
kukimwagia sifa kikosi kilichoingia
na kuwazuia Simba kufunga mabao
zaidi na wao kupata bao moja.
Alisema kuwa haikuwa Yanga
anayoifahamu katika mchezo huo
huku wachezaji wake, Hamis Kiiza,
Didier Kavumbagu na Athuman Idd
wakicheza chini ya kiwango na
kuwapa mwanya Simba kutawala
muda mwingi hasa eneo la kiungo.
"Nimemwambia Kiiza na wenzake,
soka la mdomoni kwa sasa halina
nafasi, wengine wameshindwa
kufanya kile tulichowafundisha na
kuwaagiza, walichokifanya ni
madudu na kushindwa
kutufadhaisha," alisema Minziro.
Alisema kuwa amefuraishwa na
kiwango kilichoonyeshwa na
wachezaji kama Hassan Dilunga,
Simon Msuva, Juma Abdul, Jerryson
Tegete na wachezaji walioanza, Frank
Domayo, Kelvin Yondani, Mbuyu
Twite na Haruna Niyonzima kwa
kuonyesha kuwa wanaweza.
"Angalia Okwi (Emmanuel), ameingia
na kufanya vitu vikubwa,
ameonyesha thamani yake, lakini
awali, ilikuwa tofauti, Ngassa
anapewa mpira, anajitahidi kuwahi,
lakini hakuna mtu wa kumsaidia
ndani ya mabeki watano wa Simba,
haya hayakuwa mafundisho kwetu,"
alisema.
Kuhusiana na Kaseja, Minziro alisema
kuwa ni vigumu kwa kipa
kufanyakazi za ziada baada ya
mabeki kupitwa na huwezi
kumlaumu, labda kwa bao la tatu
ambalo limetokana na uzembe.
Wakati huo huo; Uongozi wa Yanga
umeitisha mkutano wa ghafla na
waandishi wa habari utakaofanyika
kuanzia saa 4.30
asubuhi.Haijafahamika mkutano huo
utakuwa na madhumuni gani na nani
atazungumza na waandishi wa
habari.

No comments:

Post a Comment