Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 24 September 2013

LULU MPYA AZALIWA


lulu1 cb52f
IMENICHUKUA saa kadhaa kuzungumza na mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu za Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', hakika yeye ni Lulu kama lilivyo jina lake. (HM)
Kwa wakati huu msanii huyu ni lulu kweli katika tasnia ya filamu za Bongo Movie. Inaaminika kuwa binti huyo ambaye ni hivi karibuni tu alifikisha umri wa kuhesabiwa kuwa ni mtu mzima (miaka 18), naye ameingia katika kundi la wasanii wa kike wasiokamatika kwa kiwango.www.tabasamuleo.blogspot.com

Yeye ndiye Mwigizaji Bora wa Kike kwa mwaka 2012/2013 kupitia tuzo zilizotolewa na Zanzibar International Film Festival, anasema kuwa amekua kiumri na sasa yeye ni Lulu mpya mwenye majukumu ya kuelimisha jamii.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa yuko nje kwa dhamana kutokana na kukabiliwa na kesi ya kuhusika na mauaji bila kukusudia ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Alichofanya Lulu sasa ni kuzindua filamu inayokwenda kwa jina la 'Foolish Age'. Filamu hiyo ilizinduliwa
Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wa mamia ya wapenzi wa fani hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Lulu aliipongeza kampuni inayomsimamia ya Proin Promotion kwa kumpa nafasi ya kuwafundisha wengine mambo aliyopitia akiwa mtoto ambaye hakupenda sana kuwasikiliza wakubwa zake.
Lulu ni nani na aliingiaje katika filamu?
Anasema alianza kuigiza alipokuwa na umri wa miaka minne, lakini hakuwa maarufu. Alipofikisha umri wa miaka saba, alikutana na Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' katika bonaza moja ambalo pia Dk. Cheni aliaandaa Talent Show. Akiwa na mama yake alimweleza Dk. Cheni kuwa anaweza kuigiza.
Katika hilo Dk. Cheni anasema: "Nakumbuka ilikuwa pale Dar West Park, alionyesha maajabu tulipompa nafasi, yeye ndiye aliibuka namba moja. Alimpita hata Masanja Mkandamizaji aliyeangukia nafasi ya tatu."
Dk. Cheni anasema alimchukua hadi kwa uongozi wa kundi la Kaole Sanaa Group ambapo Lulu alifanyiwa usaili na kupita kwa asilimia. Jukumu kubwa la usalama wa Lulu likaachwa kwa Dk. Cheni.
Akiwa Kaole, Lulu alichagua jina la Nemu na alikubalika kutokana na uwezo wake kisanii pamoja na usafi jambo ambalo hata Herieth Samson 'Kemmy' alishikwa na mshangao baada kufungua mkoba wa Lulu.
Kemmy alishangaa kukuta vipodozi vya wakubwa ndani ya mkoba huo wakati Lulu alikuwa badomdogo, alipoulizwa vipodozi vile ni vya nani, Lulu alimjibu kwa kujiamini tu kuwa ni vyake. Kemmy anaongeza akisema: "Siku zilivyozidi kwenda mbele alibadilika na kupenda kuvaa mavazi mafupi, yaani ilifikia hatua picha zake kuchapishwa gazetini."
Kemmy anafichua kwamba jina la Lulu, msanii huyo alipewa na Salum Mchoma 'Chiki' mtunzi wa mchezo wa Tetemo aliyelifuta lile la Nemu.
"Ndoto zangu zimeonekana, wakati ninaandika mchezo wa Tetemo nikampa jina la Dhahabu lakini kwa sababu tulikuwa na uhusiano na Mr. Chuzi akaniomba nibadilishe jina ili tusiwachanganye watu maana naye alikuwa na Jumba la Dhahabu, ndipo nikampa jina la Lulu," anasema Chiki.
Ushuhuda wake
Lulu mwenyewe anasema ukiacha hayo yaliyosemwa na hao waliomkuza kisanii, lakini amepitia mengi katika maisha yake kiasi cha kumpa maumivu makubwa mama yake.
Lakini anaamini yote hayo yalikuwa njia ya kumfanya aje kuwa mtu wa kuifundisha jamii kupitia sanaa na ndiyo maana ameandaa filamu inayoelezea maisha yake akiwa chini ya miaka 18.
"Sikumsikiliza mama yangu, wakubwa zangu, nilikuwa kizani. Yale niliyoyafanya ndio niliamini kuwa ni sahihi, yaani sikuona hatari yoyote mbele yangu," anasema.
"Hata hivyo naamini ulikuwa mpango wa Mungu kwa yote yaliyotokea. Kuna walionihukumu
, lakini kwa sasa nimekua, ninampenda Yesu na mimi ni Lulu ni mpya. Lengo langu ni kuielimisha jamii kupitia sanaa yangu," anasema.
Lulu ndiye mlezi wa familia yake, ndiye anayegharimia ada ya mdogo wake anayesoma katika moja ya shule za kimataifa.
Anasema malengo yake ni kuwa mwigizaji wa kimataifa na kuitangaza Tanzania kupitia filamu. Anaamini anaweza kufanya hilo, anaomba Mungu amsaidie.
Baada ya filamu ya 'Foolish Age', Lulu anatarajia kutoa filamu ya 'Mapenzi Ya Mungu' kazi ambayo amemshirikisha mama yake marehemu Kanumba, Frola Mtegoa.
Anasema filamu hiyo, nayo bado itakuwa ikiongelea maisha na mikasa huku akisisitiza kuwa sasa hatotengeneza wala kuigiza filamu za mapenzi.
Filamu alizoigiza siku za nyuma na kumpa sifa ni 'Tetemo', 'Jahazi', 'Dira', 'Tufani', 'Gharika' na 'Baragumu'. Chanzo: mwanaspoti

No comments:

Post a Comment