Kwa sasa wamevunja rekodi ya kuwa wasanii ambao nyimbo zao hazijawahi kuachwa kupigwa kwenye majumba ya starehe tangu mwaka 2003 mpaka dakika hii unaposoma ukurasa huu.
Mwaka huo ndipo walipozindua albamu yao ya kwanza 'Last Night' ambayo ilitengenezwa na Timbuk Music Label.
Wasikilizaji wazuri wa muziki, watakumbuka kwamba tangu kutolewa kwa ngoma yao ya kwanza, kila mwaka wakali hao wanadondosha nyingine na mpaka sasa hawajawahi kupotea kwenye ramani.
Unaposoma makala haya, wimbo wao bora wa 'Alingo' unatesa na huku 'Personally' ukiendelea kupasua anga vilevile.
P-Square wametoka mbali mpaka kufikia hapo walipo sasa, kati ya mambo yaliyowawezesha
kufikia mafanikio walionayo ni pamoja na kuwa na moyo wa kupenda kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao waliowatangulia.
kufikia mafanikio walionayo ni pamoja na kuwa na moyo wa kupenda kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao waliowatangulia.
Walianza kuonyesha vipaji vyao tangu walipokuwa katika elimu ya sekondari nchini kwao Nigeria.
Waliwahi kujiunga na chama cha muziki na maigizo baada ya kupata mafunzo. Wakati huo waliimba na kucheza nyimbo za wasanii wa nje ya nchi yao kama vile Micheal Jackson, Bobby Brown na MC Hammer.
Mwaka 1997 waliunda kikundi kilichojulikana kwa jina la MMMPP, ikiwa ni majina yao na wenzao, M Clef a.k.a Itemoh, Micheal, Melvin, Peter na Paul. Kutokana na kumkubali sana Micheal Jackson, walianza kucheza Break Dance.
Mwaka 1999, P-Square walirudi katika shule ya muziki ili kujiendeleza katika mafunzo ya upigaji gitaa, kinanda, ngoma, filimbi na kadhalika. Mpaka sasa wao ndiyo wanamuziki nguli wanaomudu kupiga ala mbalimbali.
Baada ya hapo walijiendeleza na masomo katika Chuo Kikuu cha Abuja wakisomea masomo ya Utawala wa Biashara. Chanzo: mwanaspoti
No comments:
Post a Comment