NA LILIANI SETH
Mahusiano na
afya kwa hakika vinashabiana kwani vinategemeana kwa kufanya kuwepo furaha angalau kidogo kwa mwanadamu ni
wazi kama hauna mahusiano ya aina yeyote ni dhahiri afya yako itadhorota hivyo
tarajia afya njema kama unamahusiano.Mahusiano ni neno pana kulingana na uzito
na ugumu wa kuzingatia katika mahusiano na pia yapo mahusiano ya aina
mbalimbali kama kati ya wazazi na watoto wao,familia moja na nyingine,mtu na
mtu na hata shirika na shirika lakini
leo nitazungumzia mahusiano ya mtu na mtu
Ni rahisi
kujenga mahusiano na mtu yeyote lakini ni vigumu kudumisha na kufurahia
mahusiano hayo kutokana na utofauti kama
wa rika,hali ya kimaisha,tabia,imani na mengineyo mengi hivyo ni vizuri kabla
ya kuanzisha mahusiano ni lazima ukubali kuzingatia vitu Fulani ili kuhakikisha
unapokuwa na mahusiano yanadumu kwa wakati wote.Katika maisha tunayoishi
tunategemea mahusiano ili kutoa na kupokea vitu Fulani ambavyo inawezekana
vinafaida au havina faida kwa wakati mwingine vinadhoofu miili yetu
Mojawapo ya
ishara ya afya njema ni furaha japo kwa wakati mwingine mtu anaweza kuwa na
furaha ya usoni na wala si moyoni
JINSI
YAKUTENGENEZA FURAHA YA KWELI
-Kuikubali
imani yako[dini]kuwa na imani ambayo itakuongoza kutekeleza mema
-kula lishe
bora[balance diet]
-Fanya vitu
unavyofurahia[hoby kama kuogelea,kucheza,kuimba n.k
-Kuwa zaidi
ya usafi[nadhifu na wakupendeza]
-Jikubali
kabla ya mwingine kuonyesha kukubali[usitamani kuwa na maumbile ambayo ni wazi
hutoweza kuwa nayo kama ufupi,urefu n.k]
-Kubali
kusamehe wengine
-Fanya
shughuli zako za kimaisha kwa bidii[ikiwa ni kazini,shule na hata nyumbani]
-Jisikie
kuwajali,kuwapenda,kuwathamini na hata kuwasaidia wengine
Ni dhahiri
furaha ya kweli haihitaji ubinafsi ni lazima kuwepo sababu ya mwingine kuongeza
furaha yako japo kama kwa mazingira Fulani inawezekana kutokuwepo mtu wa
kuongeza furaha yako kwa kuona hivyo unawajibu wa kuzingatia zaidi
niliyoyazungumzia hapo juu ili kuhakikisha unaendelea kuwa na afya njema
Mahusiano ya
mtu na mtu inawezekana yakawa ya mwanaume na mwanamke[msichana na mvulana na
hata jinsia moja]
Japo watu
wengi hawajali na wala kuumizwa na mahusiano ya jinsia moja na hii ni kwasababu
mahusiano ya jinsia tofauti yanalenga uhitaji zaidi kwa kutoa na kupokea kitu
zaidi ya kawaida,neno kawaida ni hali ya mazoea na mtu wa aina yeyote wala
uzingatiaji wa kitu chochote hauhitajiki
Kama upo
uhusiano wa jinsia tofauti ni wazi kipo kitu zaidi ya kawaida na ni lazima vipo
vitu vya kuzingatia ili isije ikawa ni kawaida.Mahusiano yanahitaji vitu
vitatu[3]pekee
-Akili
-Moyo
-Mwili
Na kwa
hakika vinatakiwa kulingana na wala siyo kingine kuzidi kwa mwenzake kwani kwa
kuzingatia hivyo tunaweza kuhifadhi furaha ya kweli,Akili ni uwezo wa kufikiri
na kupambanua jambo na moyo ni uhifadhi kwa yaliyo mazuri na hata mabaya lakini
mwili ni ukubali wa viungo vya nje na ndani ya mwili kufanya kazi hivyo ili
kuwepo kwa afya njema hutegemea utendaji mzuri wa akili,moyo na mwili na
Vyote hivyo
vipo ndani maamuzi yetu kwa ruksa ya mwenyezi mungu pekee hivyo tunawajibu wa
kuvitumia tunavyotaka lakini matokeo ni jibu la utumiaji mzuri au mbaya vitu
hivi.jiulize ni kwanini unapokea maumivu katika mahusiano ikiwa umepewa uwezo
wa kutawala vitu hivi vitatu inawezekana ni uzembe wakutozingazia ulinganifu wa
vitu hivi.
Ni wazi kila
mmoja anatamani kuongeza furaha kwa kuwa katika mahusiano kwa kupitia blog hii
inawezekana kuamua kupata mahusiano sahihi na yatakayokidhi malengo yako
NAMNA YA
KUTUMIA AKILI,MOYO NA MWILI KATIKA MAHUSIANO
-AKILI
katika mahusiano inatumika katika
kufikiri kwamba Yule unayetamani kuwa na mahusiano naye mnashabiana
kitabia,rika,hali ya maisha na mengineyo japo mengine hayana umuhumu kwa
kuzingatia makubaliano ya wanamahusiano
-Moyo ni
sehemu ya mahusiano kwa kupitia mbinu mbalimbali unaweza kutambua nguvu ya
hisia ulizonazo kwa unayemkusudia kuwa na mahusiano naye
-mwili pia
huwakilisha na kutimiza yatakayo moyo hivyo ni lazima ukubali vitu hivi kufanya
kazi pamoja bila upendeleo ili kupata kitu timamu
Mahusiano ni
jambo la hiyari lakini ni muhimu ili kuendeleza na kutunza furaha ya kweli na kwa
kuzingatia yote hayo ni rahisi kuepuka mahusiano ya haraka na gafla
Namalizia
kwa maswali ambayo nahitaji uyajibu bila mimi kusikia
-UNGE PENDA KUONGEZA
FURAHA?
-JE
UNAWEZA KUISHI BILA MAHUSIANO YEYOTE?
- JE UNAWEZA
KUJARIBU KULA,KULALA,KUTOZUNGUMZA NA MTU YEYOTE?
-JE UNAWEZA
KUISHI MAISHA YA PEKE YAKO BILA KUTOA
WALA KUPOKEA CHOCHOTE KWA MWINGINE?
- JE UNAWEZA
KUISHI SEHEMU AMBAYO UNAWEZA KUPATA
VITU VYOTE ISIPOKUWA KUMUONA
MTU WA JINSIA YEYOTE ?
MWANDAAJI WA MAKALA HII NI LILIANI
SETHI
No comments:
Post a Comment