Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 28 October 2013

Mgengwa; LEO NIMEONGEA KWA SIMU NA PRESIDENT MALINZI NA NYAMLANI...



Ndugu zangu,
Kwa nafasi yangu ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu, TFF, katika nyakati tofauti, leo niliongea kwa simu na Rais mpya wa TFF Ndugu Jamal Malinzi na aliyemshinda kwenye nafasi ya Urais Ndugu Athumani Nyamlani.
Nimempongeza Ndugu Malinzi kwa ushindi wake. Vile vile, kama mwanafamilia ya mpira, nimemwahidi President Malinzi ushirikiano wangu katika juhudi zake za kufanikisha malengo ya TFF ikiwamo kumsaidia kwenye kufanikisha utekelezaji wa ahadi zake kama mgombea.
Wakati huo huo, kwa njia ya simu nimeongea na Ndugu Nyamlani na kumpa pole ya kushindwa.
Nimemwambia, kuwa maisha ya mpira yanaendelea na kuwa , kutokana na uzoefu mkubwa alioupata akiwa kiongozi TFF, na kwa vile bado ni kijana, basi, kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania bado utatarajiwa mchango wake kwa njia moja au nyingine.
Nachukua fursa hii pia kuwapongeza wagombea wote walioshinda kuingia kwenye Kamati ya Utendaji.
Na kwa walioshindwa wasikate tamaa.
Mpira utaendelea kudunda...!
Maggid.
Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment