Jibu langu ni hili:
Hii sio ya kitaalamu bali ni mimi ninavyofanya na ndio inayonisaidia kupunguza tumbo.
Kwasababu vitu vya formula mimi huwa siwezi kuvifuata na huwa naviona vigumu sana kwahiyo huwa najaribu kuishi vile ninavyoweza.
Na kizuri zaidi ni kwamba hii sio diet ya kujinyima.
Ila unaweza usifanikiwe pia kutokana na mwili wako kwakua tumeumbwa tofauti lakini unaweza kujaribu kama itafanya kazi

Na nikiisha amka nakunywa maji ya uvugu vugu yaliokamuliwa ndimu au limao glass zingine tatu kabla ya kunywa Chai.
Ukizoea maji ni matamu kuliko hata biere
Kuwa Teja wa Maji kuna raha yake pia

Ukiweza kunywa maji ya uvugu vugu kila wakati unapohisi kiu ya maji itakuwa vizuri au hata mara tatu kwa siku angalau




Kumbuka mimi huwa sifanyi diet hivi ndivyo ninavyokula na inasaidia

Mara nyingi usiku naipotezea tu, pengine nalalia glass 2 za wine au beer kadhaa zisizozidi 3
Au Kuku wa kienyeji wa kuchemsha aliewekwa chumvi na ndimu na ka ndizi kamoja ka kuchemsha au kukaanga kwa mafuta kidogo sana

Lakini kumbuka wanga sio kitu cha kukiendekeza sana hasa unapotaka kutoa kitambi
Nikiona kinachomoza, napunguza maswala ya ugali.
Japo kwangu ni ngumu siku ipite bila Ugali, ila kumbuka miili inatofautiana... naweza nikala ugali mwaka mzima mwingine akala wiki akafumuka
So usinifatishe ila jaribu kupunguza au uepuke kama utaweza

Hili ndio tatizo lililonikuta mpaka mkaona ile ishu imechomoka siku ya Birthday yangu
Kwakweli chips ni tamu hasa kwa sisi tunaofanya kazi za usiku ukirudi umejichokea unavamia tu
Unakuta unafululiza hata mwezi unazila kisha unaenda kulala
Japo tunapenda chips vumbi ila tuwe na kipimo isizidi, isiwe kila siku
Ukijumlisha na bia, daaah!! dah!!!!!! dah!!!!! shughuli imeisha
No. 1 enemy kwa vitambi vya wanawake ni hii kitu
Kula angalau mara moja kwa wiki tafadhali kama huwezi kuacha kabisa
Wenye kuweza kufanya sit ups pia fanyeni japo najua mazoezi ni magumu sana na yanatia uvivu hasa unapokuwa na kazi nyingi
Maji ni kitu cha lazima na cha kila siku
Ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu Asubuhi, Mchana na Usiku utafanikiwa japo kidogo
Narudia hii sio Diet ya kitaalam ni jinsi ninavyo ishi mimi, jaribu kama utaweza kufanikiwa kwa wale walioniomba ushauri.
Ila kama mwili wako ni mkubwa sana pia jaribu kupunguza kipimo cha chakula unachokula kila siku, ila usijinyime sana.
Mboga mboga kibao kila siku ukiamua mchana na jioni. Ni muhimu sana
with love
Binti Machozi
No comments:
Post a Comment