Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday, 7 October 2013

FIESTA AU MAJANGA? CHANGIA MAONI YAKO TUYAFIKISHE KWA WAZIRI MWENYE DHAMANA...!



Juma la jana niliandika hivi;

Majanga Haya! Ningelikuwa Waziri Wa Vijana, Utamaduni Na Michezo...

Basi, Siku ya kwanza tu ya kuingia ofisini ningetoa tamko la kupiga marufuku fiesta zote isipokuwa kwenye misimu ya likizo za wanafunzi. Na kwa masharti, kuwa fiesta kwa watoto chini ya miaka 18 zianze alasiri na kumalizika saa kumi na mbili jioni. Fiesta za usiku iwe ni kwa watu wazima tu.

Tuwe wakweli kwa jamii yetu na Nchi Yetu. Wanaosema ' Twenzetu tukawinde' wanapotosha umma. Ni sawa na kusema pia ' Twenzetu tukawindwe'. Wahenga walinena; mwinda huindwa. Hapo pichani imeandikwa, kuwa bia laki 2 kuwindwa. Ni majanga. Hapa kuna ' wawindaji haramu' wenye kuwaaminisha wenye kuwindwa kuwa wao ndio wawindaji! 


Ina tafsiri ya vijana wetu na hususan walio mashuleni ndio wenye ' kuwindwa' na watengenezaji wa vilevi. Halafu tunashangaa kuwa matokeo ya form four ni mabovu kila mwaka unaoingia wakati fiesta hizi zinawapagaisha vijana wetu wengi na kuacha ku-focus kwenye masomo yao.

Ndio, ni wazazi pia wenye ' kuwindwa'. Na hawana pa kusemea. Fiesta hizi zinawaweka roho juu wazazi. Kuna wasichana wenye kubakwa kwenye giza la fiesta na umati wa vijana wengine waliolewa na hata kuvuta bangi. Nani anajali?

Tulipofika ni pabaya. Inatosha kuwa kwa sasa tuna hata vijana wetu wanaoingia darasani na 'viroba' vya pombe mifukoni. Naambiwa mwanafunzi anafyonza kiroba huku akimsikiliza mwalimu. Haya ni majanga ya kujitakia.

Na ipigwe sasa MARUFUKU ya FIESTA kwenye misimu ya masomo. Ipigwe pia marufuku ya viroba kuuzwa kwenye maduka ya mitaani isipokuwa kwenye sehemu za vilevi na kwa kuzingatia umri.

Na kinachosikitisha hapa ni kuona vijana wetu wakiangamia kupitia hata hayo yanayoitwa ' matamasha ya muziki'. Mengi hugeuka kuwa ' matamasha ya ulevi na ngono zembe'. Ni majanga, kama wanavyoita mitaani.
Tuvunje Ukimya.
Maggid Mjengwa.
0754 678 252www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment