Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage
UONGOZI wa Simba, umetuma malalamiko yenye kurasa 11 kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) wakitaka kulipwa fedha za mauzo ya Emmanuel Okwi kutoka kwa klabu ya Etoile du Sahel.
Okwi aliuzwa na Simba kwa klabu hiyo ya Tunisia Januari mwaka huu kwa gharama ya uhamisho wa Dola za Marekani 300,000 (Sh480 milioni), ambazo kwa mujibu wa makubaliano zilipaswa kulipwa kufikia Septemba 30, lakini Etoile haikufanya hivyo.
Pia, mshambuliaji huyo naye anaidai Etoile malimbikizo ya mshahara wake pamoja na gharama za usumbufu na ndiyo sababu akasusa na kurudi kwao Uganda ingawa mwishoni mwa mwezi huu alikuwa jijini Dar es Salaam kwa mishemishe zake.
Katika malalamiko hayo yaliyotumwa juzi Alhamisi, kurasa tatu za mwanzo ni maelezo ya malalamiko yao na kurasa nane zingine ni viambatanisho vya maelezo mbalimbali vinavyoonyesha makubaliano baina ya klabu hizo mbili wakati wanauziana mchezaji huyo.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Tumechukua hatua ya kupeleka malalamiko yetu Fifa yenye kurasa 11 kati ya hizo tatu ni maelezo ya barua husika na nane ni vielelezo mbalimbali.”www.tabasamuleo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment