Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 10 October 2013

Ebwana hii ndio stori nzima kuhusu hii vita ya maneno Twitter kati ya Jack Wilshere na Kevin Pietersen




Kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya England Jack Wilshere amepinga wazo la kutoa uraia kwa wachezaji wasio na asili ya England na kutoa fursa ya kuichezea timu ya taifa ya England .

Wilshere alizungumza hayo wakati anajibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mawazo ya kocha wa England Roy Hodgson ambaye amevutiwa na kipaji cha kiungo wa Manchester United Adnan Januzaj hadi ya kufikiria kumshawishi aichezee England .

Wilshere amesema kuwa England inapaswa kuwakilishwa na wachezaji waliozaliwa England pekee na si wahamiaji kwa kuwa hawawezi kuwa na asili ya utaifa kama waliyo nayo wachezaji waliozaliwa England .

Mawazo ya Wilshere yamepingwa na kocha wa timu ya taifa ya vijana ya England Gareth Southgate ambaye kikosi chake kina wachezaji watano ambao sio wazaliwa wa England .

Jamii ya wanamichezo ya England ikiongozwa na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cricket ya Ungereza Kevin Pietersen imempinga vikali kiungo huyo wa Arsenal kwa kile kinachoonekana kama ubaguzi .

Pitersen ambaye sio mzaliwa wa England alizaliwa nchini Afrika Kusini lakini aliiwakilisha England na kuipa mafanikio makubwa kwenye mchezo wa kriketi.  www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment