Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 12 October 2013

Refa wa Fifa kuchezesha Simba, Yanga



Mwamuzi Israel Nkongo akitolewa uwanjani na polisi wa kikosi cha FFU mara baada ya kutokea vurugu mwaka jana.Picha na Maktaba

MWAMUZI Israel Nkongo wa Dar es Salaam amepangwa kuchezesha mechi ya Simba na Yanga itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa, Oktoba 20.

Nkongo, ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Fifa, alipigwa na wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephano Mwasyika na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, katika mechi ambayo Azam walishinda 3-1 wakati timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 10 mwaka jana.

Nkongo alipata balaa jingine baada ya kuondolewa dakika za mwisho kuchezesha mechi ya mwisho wa msimu uliopita kati ya Simba na Yanga, Mei 18 mwaka huu na mechi hiyo ikachezeshwa na Martin Sanya wa Morogoro na kushuhudia Yanga ikishinda mabao 2-0.


Kuondolewa kwa Nkongo katika mechi hiyo ya mwishoni mwa msimu uliopita, kulitokana na ushauri wa ofisa usalama wa Fifa kushauri kuwa iwapo angechezesha mwamuzi huyo, Yanga wangeweza kufanya vurugu kutokana na Yanga kudai alivuruga mechi yao dhidi ya Azam.


Nkongo alisababisha Mwasyika kufungiwa mwaka moja na kulipa faini ya Sh milioni moja kutokana na kosa hilo huku Jerry Tegete akisimamishwa kwa miezi sita na wengine kama Cannavaro, Omega Seme na Nurdin Bakari wakifungiwa mechi tatu na kila mmoja kutozwa faini ya Sh500,000.


Baada ya kupita vizingiti vyote hivyo, Mwanaspoti linaweza kuthibitisha kuwa sasa Nkongo atakuwa katikati katika mechi ya watani itakayopigwa Oktoba 20.


Hata hivyo, haitakuwa ajabu iwapo ofisa usalama wa Fifa akishauri tena kuwa mwamuzi huyo abadilishwe tena kutokana na kuhisi kuwa Yanga wanaweza kumkataa.   www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment