Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 10 October 2013

ROONEY;BADO NINAHITAJI KUCHEZA NAFASI YA USHAMBULIAJI



Mshambuliaji wa man U, Wyne Rooney

Mshambuliaji wa manchester United Wyne Rooney amezidi kusisitiza anahitaji kucheza nafasi ya mshambiliaji wa kuongoza mashambulizi katika timu hiyo ya mashetani wekundi yeynye maskani yake jijini manchester.akizungumza na waandishi wa habari rooney amesama,,


"Kila mmoja ndani ya klabu anajua ninataka kucheza nafasi gani pindi niwapo uwanjani,na wanajua kwa nini nilivunjika moyo hapo awali,niliambiwa nicheze nafasi ya kiungo,nilikwenda lakni sikupenda kucheza pale

"Ukweli nilipocheza kwenye nafasi ya kiungo nilifanya vizuri lakini sikupenda kucheza nafasi hiyo,sikuw na tatizo awali la kucheza lakini kwa sasa nahitaji kucheza nafsi ninayoitaka

"Kihalisia inakatisha tamaa lakini labda kuendana na michezo fulani inahitajika mimi kucheza nafasi ya kiungo

"Wakati mwingine nakwenda kucheza kwenye nafasi yangu,n wakati mwingine inakuwa ngumu ninaporudi kwenye nafasi yangu

"Kwa kuwa mwaminifu nilikuwa nimetulia msimu mzima uliopita,nilikuwa nafuraha muda wote wa msimu kwa mtazamo wa nje hili halikuonekana lakini ukweli nilikuwa nimetulia

"Mke wangu amepata mtoto mwingini ni jambo la kufurahia pamoja na kwa sasa nikiwa nasumbuliwa na tatizo la jeraha la kichwa,nazidi kulishughilia kwa umakini na kuwaonesha watu wote duniani kuwa mii ni mchezaji bora duniani

"Siwezi kuja hadharani na kusema nataka kuondoka au nataka kuendele kubaki,ninachotakiwa kufanya ni kujishughulisha na maswala ya mpira na kusubiri nini kitakachotokea

"Unaweza ukaniona nina furaha kwa nje lakini bado nipo kwenye mazungumzo na klabu ili kufahamu nini watakifanya dgidi yangu mimi.

"Timu imebadilika hasa kwa ujio wa kocha mpya na uongozi mzima wa bench la ufund,

"Mazoezi ni magumu,ninakimbia sana

"Hili linanisaidia sana,najihisi vizuri kuliko wakati wote wa uchezaji wangu,ni vitu mchanganyiko,najihisi furaha na kufurahia kazi yangu ya mpira."

No comments:

Post a Comment