Kundi la Jahazi Modern Taarab kama kawaida yake Jumamosi iliyopita lilifanya makamuzi ya aina yake ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuwanogesha maelfu ya mashabiki waliofurika ukumbini humo.
Umati huo wa mashabiki karibu muda wote ilikuwa ni mambo ya kukatiana nyonga usiku kucha hali iliyosababisha mashabiki hao kuomba onesho hilo lirudiwe ukumbnini hapo hivi karibuni.
Kama kawaida ya uwanja huo wa burudani kulikuwa na matukio mengi ya kiburudani ikiwemo michezo ya kushindana kuendesha baiskeli, kubembea, kupanda ndege na mingineyo.
Naye muimbaji wa kundi hilo, Ustaadh Amigo alinogesha mambo kwa kufanya sherehe yake ya kutimiza miaka 43 tangu kuzaliwa.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS www.tabasamuleo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment