Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 12 October 2013

Taarifa kuhusu ishu ya Henry Joseph wa Simba


Imefahamika kwamba kiungo mkongwe wa Simba Henry Joseph ataendelea kubaki kwenye timu B na huo ni uamuzi wa benchi la ufundi la timu hiyo.
Kocha Msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelo anasema Henry atabaki hapo hadi atakapobadilika ‘anatakiwa kubadilika na kuonyesha juhudi kwamba alikuwa anacheza nje basi atuonyeshe kweli anastahili kuwa katika timu ya kwanza na atatoa msaada’
“Hatujapenda vyombo vya habari kuandika vitu tofauti kama vile kufukuzwa Simba na vinginevyo, tulichofanya ni kwa manufaa ya Simba, kama Henry angekua anajituma wala kusingekuwa na tatizo, tunajua alikuwa Ulaya na ndio maana tunategemea mchango mkubwa kutoka kwake’ – Julio.
Henry alizuiwa kuendelea na mazoezi na Kocha Mkuu Abdallah Kibadeni baada ya yeye kuanza kuomba apumzike, Kibadeni alimwambia aendelee kupumzika baada ya kiungo huyo kurudi uwanjani na kutaka kuendelea na mazoezi.
Kabla ya hapo Henry aliomba kupumzika kwa madai alikuwa amefanya mazoezi binafsi hivyo kuusikia mwili hauna nguvu ila inaelezwa alijichanganya kwani awali alimwambia Julio anajisikia mgonjwa halafu akamueleza Kibadeni kwamba alikuwa amechoka kutokana na mazoezi.
Kibadeni akamwambia akaendelee kupumzika kwenye gari kama alivyokuwa amekaa hapo awali.

No comments:

Post a Comment