Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday 6 October 2013

PATA Matokeo kamili ya English Premier League.




Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea hii leo baada ya michezo sita iliyopigwa hapo jana.

Katika michezo ya hii leo Chelsea waliwafunga Norwich City kwa mabao matatu kwa moja .

Chelsea walifunga kupitia kwa Oscar , Edin Hazzard na Willian huku Anthony Pilkington akifunga bao pekee la Norwich .

Katika mchezo mwingine Southampton waliendeleza mwanzo wao mzuri wa ligi baada ya kuwafunga Swansea City kwa mabao mawili bila.



Wafungaji wa Southampton walikuwa Adam Lallana na Jay Rodriguez.

Arsenal waliokuwa wanatafuta kuendeleza rekodi ya kushinda kwenye mechi zaidi ya 10 walisimamishwa na West Bromwich Albion ambao waliwalazimisha vijana hao wa Arsenal Wenger sare ya 1-1 . West Brom ndio walioanza kufunga kupitia kwa Claudio Yacob lakini Jack Wilshere alisawazisha bao hilo .





Katika mchezo mwingine uliopigwa leo Tottenham Hotspurs walipoteza mchezo wa pili kwa msimu huu baada ya kufungwa na West Ham United 3-0 . United walifunga mabao yao kupitia kwa Ricardo Vaz Te ,Ravel Morrison na Winston Reid.www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment