Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday, 27 January 2014

CHELSEA YAIPIGA BAO LA KISIGINO MAN UNITED KWA DIEGO COSTA

KLABU za Chelsea na Atletico Madrid zimekubaliana kubadilishana wachezaji, Diego Costa ahamie Stamford Bridge msimu ujao, kwa mujibu wa vyombo habari Hispania.
Kipa wa Blues, Thibaut Courtois, anayecheza kwa mkopo Atletico, amekuwa akizungumziwa na wengi kama mlinda mlango hodari kinda Ulaya, baada ya kudaka vizuri akiwa na klabu hiyo ya Hispania kwa misimu mitatu.
Lakini kipa huyo mwenye umri wa miaka 21 angependa kubaki Madrid, na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anamtaka mshambuliaji nyota, Costa arejee. Kocha wa Manchester United, David Moyes alitumai kumpata mshambuliaji huyo Old Trafford.

Karibuni atakuwa wa Blue? Diego Costa anaweza kuwa njiani kuelekea Stamford Bridge


Vidole gumba juu: Kwa vyovyote, kipa Thibaut Courtois anayedaka kwa mkopo wa muda mrefu Atletico, atahamia moja kwa moja klabu hiyo
Costa amefunga mabao 19 katika La Liga msimu huu, akishika nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Cristiano Ronaldo wa Real.
Kipaumbele cha Mourinho katika usajili huu ni mshambuliaji, na Mreno huyo amegoma kuondoka Januari.
Chelsea ilitaka kipa Courtois asaini Mkataba mpya licha ya kwamba hajawahi kuchezea timu ya Stamford Bridge, lakini Mbelgiji huyo angependa kuchezea klabu kwa Mkataba wa kudumu badala ya mkopo.
Courtois awali alisema atarejea Chelsea tu kuwa kipa namba moja mbele ya Petr Cech.

No comments:

Post a Comment