Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 2 December 2013

Matola: Simba, Yanga badilikeni

KOCHA wa kikosi cha Simba B, Selemani Matola, amezitaka klabu za Simba na Yanga kuachana na mtindo wa kusajili wachezaji wale wale na sasa zijikite kuwapandisha vijana kutoka vikosi vya vijana.
Matola ameliambia Mwanaspoti kuwa kuna haja ya klabu hizo kubwa nchini kuona ni jinsi gani zinawasajili vijana badala ya kuendelea na mfumo wa kubadilishana tu wachezaji bila ya kufanya usajili wa maana.

“Yanga wanamtema mchezaji fulani, Simba wanamsajili, baadaye Simba inamtema, Yanga inamchukua...ndio maana soka halikui,” alisema Matola.


Kocha huyo ambaye aliteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Simba kuwa Kocha Msaidizi ya timu ya wakubwa, aliongeza: “Tukiwekeza kwa vijana hatutapata taabu ya kusajili, pengine gharama zingine zisizo za msingi hazitahitajika.


“Hiyo tabia ya klabu za Simba na Yanga kusajili wachezaji kwa kubadilishana na mpaka kipindi mchezaji anaacha soka unakuta amezunguka kwenye klabu hizo zaidi ya mbili.


“Mfano mzuri wa mchezaji aliyecheza timu hizo mara mbilimbili ni Athumani Idd ‘Chuji’ na Juma Kaseja, najua pia kwa inatokana na ubora wao, ingawa si sahihi sana. Timu hizi zikiwekeza kwa vijana lazima zitakuwa na wigo mpana wa kusajili wachezaji.”


Chuji alisajiliwa na Simba, baadaye akajiunga na Yanga kisha akarudi Simba na sasa yuko Yanga. Kaseja naye alifanya vivyo hivyo na sasa amesajiliwa tena kwa mara ya pili na Yanga.

No comments:

Post a Comment