Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 3 December 2013

ZANZIBAR HEROES YAPIGWA NA KENYA - HATARINI KUAGA MASHINDANO YA CHELLENJI




Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe.COMMICHUANO ya kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA Challenge imezidi kushika kasi leo nchini Kenya ambapo wenyeji Kenya wameungana na Wahabeshi wa Ethiopia kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifumua Zanzibar Heroes mabao 2-0, Uwanja wa Afrah, Nakuru.

Alikuwa ni Beki wa Azam fc, inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara, Joackins Atudo aliyekuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza dakika ya 6 na baadaye mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga akaandika kimiani bao la pili dakika ya 60.
Kwa matokeo ya leo, Zanzibar inabaki na alama zake tatu na sasa wapo mguu ndani-nje kwani watasubiri hatima ya kwenda robo fainali katika nafasi mbili za `Best Losers`.

Kwa Harambee Stars mambo yamejipa yenyewe kwa kutinga robo fainali kwani wametimiza alama 7 baada ya awali kuwalaza Sudan Kusini mabao 3-1 na kutoka suluhu na Ethiopia.

Mchezo mwingine wa kundi A uliopigwa mapema uliwakutanisha Sudan kusini dhidi ya Ethiopia na kushuhudia dakika tisini zikikamilika kwa wahabeshi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa Afrah mjini Nakuru, Kenya.

Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Yousuf Yassin aliyetokea benchi kipindi cha pili na kufunga bao la kwanza dakika ya 54 baada ya kupokea pasi nzuri ya Manaye Fantu kutoka upande wa kulia na Biruk Kalbolre aliyeingia pia kipindi cha pili na kufunga goli muhimu dakika ya 82.

Sudani Kusini sasa linakuwa Taifa la kwanza kutoa mkono wa `Bai Bai` katika michuano ya mwaka huu bila hata kupata pointi moja, kwani walifungwa mechi zake mbili za mwanzo, 2-1 dhidi ya Zanzibar na 3-1 kutoka kwa wenyeji Harambee stars.

Kesho shughuli inaendelea kwa timu za kundi B, ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars itajitupa uwanjani katika mchezo muhimu sana dhidi ya Burundi na Zambia watakabiliana na mabaharia wa Somalia. www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment