Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 26 October 2013

SOKA, MABINTI WA KIBONGO (TANZANITE) WAWAFUMUA MSUMBIJI 10-0 TAIFA

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0.

Neema Paul kushoto akishangilia na Theresa Yona baada ya kuifungia bao la kwanza Tanzania katika ushindi wa 10-0 jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa.
Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.

Wachezaji wa Tanzania wakishangilia mabao 10-0


Shelder Boniface akichezewa rafu na beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita



Winga wa Tanzania, Theresa Yona akimtoka beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita



Theresa amepiga krosi



Shelder Boniface alifunga bao tamu sana, akipiga chenga mabeki watatu na kipa wao

Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa.
Kipindi cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona.
Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah.
Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.


Kiungo wa Tanzania, Amina Ali akipambana na kiungo wa Msumbiji, Deolinda Gove



Theresa Yona alikuwa mwiba mkali leo kwa Msumbiji



Amina Ali akiwaonyesha kazi wachezaji wa Msumbiji



Kikosi cha Msumbiji leo



Kikosi cha Tanzania leo

Mashabiki wakiisapoti timu ya Tanzania leo
Tanzanites walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Dakika ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena, ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania bao la 10 dakika ya 90.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel, Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa Yona.
Msumbiji; Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice Assane dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda Gove, Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na Onesema David.

No comments:

Post a Comment