Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday, 20 October 2013

ADNAN JANUZAJ: MJUWE HUYU; ANAMILIKIWA NA MAN UNITED, ANAFUKUZIWA NA ENGLAND...MTOTO WA WAKIMBIZI WA VITA KOSOVO ALIYEZALIWA BELGIUM


Mjadala unaohusu ni nchi gani ambayo Adnan Januzaj anapaswa kuchagua kuichezea umeshika hatamu nchini England kuliko sehemu nyingine yoyote.

Wiki iliyopita kituo cha TV cha Albania kilikuwa na mjadala kuhusu nyota huyo wa Manchester United katika kipindi walichokipa jina la Hero or Traitor (Shujaa au Msaliti), kwa mtazamo atakuwa shujaa akiichagua nchi hiyo au msaliti atakapoikacha na kuchagua sehemu nyingine.

Kinda hilo lenye miaka 18 ambaye amepata umaarufu mkubwa hivi karibuni baada ya kufunga mabao mawili ya ushindi wa klabu yake ya Man United, lipo kwenye presha ya kuamua nchi gani achague kuitumikia.

Alizaliwa Brussels - Belgium, Januzaj ni mtoto wa wazazi wa kutoka Kosovo na Albania ambao walikimbia mji wa Balkan-Kosovo kuepeukana na umaskini na ubaguzi wa kidini ulioleta machafuko., jambo ambalo liliwakumba wanafamilia wengine wa ukoo wa Januzaj. Leo utafahamu historia yao kiundani.

Historia ambayo inaonyesha kwamba Januzaj anaweza kuichezea Belgium, Albania, Kosovo, Turkey au England, na mpaka leo Januzaj hajaweka wazi ni wapi jezi ya taifa gani angependelea kuivaa, hata baba yake Abedin nae amekuwa kimya.

Wakala wa Januzaj, Dirk de Vriese, amesema hakuna mwanafamilia atakayezungumza lolote mpaka watakaposaini mkataba mpya na United, ingawa bado wapo kwenye mazungumzo huku vilabu vingine vikimtolea macho kinda hilo.

Inadhaniwa kwamba kama Kosovo ingekuwa inatambuliwa na FIFA - basi Januzaj angelichagua taifa hilo, lakini sasa inaaminika England ndio wana nafasi kubwa ya kumtwaa kiungo huyo.

FA wanaamini hilo linawezekana na wameanza kuangalia kama uwezekano wa kumpatia passport ya UK itapelekea FIFA kubadili kanuni za uraia wa ukazi, inayotoa ruhusa kwa mchezaji aliyekaa ndani ya taifa moja miaka 5 mfululizo kulichezea taifa hilo.......

Januzaj, ni mtoto aliyelelewa kwenye misingi ya imani ya dini ya kiislam, yenye kufuata maadili ya dini hiyo.

Kuanzia kwa walimu wa zamani wa soka mpaka wa shuleni, hakuna kati yao mwenye jambo baya la kumzungumzia kinda hilo wala familia yake. Hata Anderlecht, klabu ya soka kutoka jijini Brussels ambayo ilimpoteza mchezaji huyo akiwa na miaka 16 kwa kumuuza kwenda United kwa sababu sheria za Belgium zinakataza kuwapa mikataba ya kazi watoto chini ya umri wa miaka 18, bado inamtakia mambo ya kheri kijana huyo.

‘Hatuna furaha tumempoteza mchezaji kwa €300,000, ada ya uhamisho ambayo ilipangwa na FIFA, hivi sasa ana thamani ya 20 million,’ msemaji wa Anderlecht David Steegen alisema.

‘Alizaliwa Brussels, alisoma katika klabu yetu, ni mmoja wetu na inatusikitisha kuona hayupo nasi. Lakini tuna furaha Adnan anafanya vizuri. Ni kijana mzuri.’

Nchini Belgium kuna taarifa kwamba United ililipa kiasi cha ziada cha €200,000 kwa familia ya Januzaj na imewapa nyumba nzuri katika moja ya sehemu nzuri ndani ya jiji la Manchester ambapo mchezaji huyo anaishi na mama na baba yake.

David Steegen, bado anakiri kwamba Anderlecht iliwafanyia klabu ya RWDM Brussels FC kitu ambacho United ilikuja kuwafanyia miaka minne baadae. RWDM ni klabu iliyokuwa ndani ya eneo ambalo familia ya Januzaj ilikuwa ikiishi pembezoni mwa jiji la Brussels - Mzee Abedin Januzaj alikuwa akimchukua mwanae Adnan na kumpeleka mazoezini baada ya kutoka alipokuwa akifanya kazi katika kampuni ya Chevrolet-Opel dealership ambapo alikuwa akifanya kazi kama mhasibu.

‘Tuliona mapema kwamba Adnan angekuwa mchezaji mzuri,' anasema Jean-Paul Pira, ambaye ndio mwalimu wa timu ya watoto chini ya miaka minne katika klabu ya RWDM. ‘Hakuwa mchezaji mkubwa sana - alikuwa sio mwenye nguvu sana - lakini uwezo wake wa kiufundi ulikuwa hauelezeki, haukuwa wa kawaida. Katika mchezo mmoja wa under 10 nakumbuka alifunga mabao 16 au 17 katika ushindi wa 22-0.'

Pira pia anamkumbuka baba yake Adnan. ‘Siku zote alikuwa mtulivu na mwenye kumsapoti mwanae, lakini hakuwahi kumsifia namna alivyocheza vizuri.’

RWDM FC haikupokea hata senti tano kutoka Anderlecht. ‘Zero!’ alisema Pira. Lakini tena, bado timu hiyo ina mapenzi na Januzaj.

Abdel Jaichi ambaye alikuwa mwalimu wa michezo wa Januzaj katika shule ya Athenee Royal De Jette iliyopo katika kitongoji cha Koekelberg kwa miaka minne ana furaha kubwa na mafanikio ya Januzaj. Alimfundisha Januzaj tangu alipokuwa na miaka 12 mpaka alipohamia Manchester akiwa na miaka 16. 'Alikuwa ni kijana mtulivu mwenye heshima ambaye alikuwa mfano mzuri kwa wenzake. Alikuwa na bidii sana katika masomo na michezo’.

‘Adnan alikuwa mchezaji bora na mwenye kipaji kuliko wenzie shuleni lakini hakuwa mbinafsi,' alisema Jaichi. ‘Alikuwa akicheza na kuwatesa sana mabeki na kujaribu kutumia nafasi alizopata kufunga mabao. Lakini pia hakuwa na shida kwenye masomo yake.’

Sir Alex Ferguson alimzungumzia Januzaj kama ‘a beautifully balanced player’, wakatik kocha wa timu ya vijana ya Anderlecht - Yannick Ferrera - amemfananisha na Johan Cruyff. Pia imefahamika kwamba amezaliwa siku moja na Cristiano Ronaldo na Neymar: February 5.

Wengi wanasema baba yake Januzaj ndio nguzo kuu ya kipaji hicho, mmojawapo ni mchezaji mwenzie wa Anderlecht Michael Heylen, ambaye kwa sasa yupo Courtrai, alisema: ‘Januzaj ni mchezaji ambaye mwenye kipaji kikubwa ambacho nimewahi kukishuhudia na kucheza nae. Alikuwa na kasi na mwenye uwezo wa kuchambua mabeki na kuwapita.
‘Lakini ikiwa Adnan alipocheza vibaya, baba yake alimuweka chini na kumkosoa na kumuelekeza pamoja na kumtia moyo wa kuongeza juhudi. Muda mwingine alikuwa mkali sana na ungeweza kumuona Adnan akilia. Lakini nilikuwa najua kwamba Baba yake alikuwa anajua nini anafanya. Alimfundisha mwanae namna ya kupambana na hilo limemsaidia katika kujij


Wakati baba yake Januzaj Abedin alipoichukua familia yake na kukimbia Kosovo, baadhi ya ndugu zake waliingia jeshini kupigania uhuru wao dhidi ya waserbia.

Lakini mpaka sasa mahusiano yao bado ni imara sana, huku kila anapopata mapumziko Januzaj, ambaye anaongea kialbania vizuri sana hutembelea nchi hiyo kwa wiki kadhaa, eneo ambalo lipo katika milima inayotenganisha Kosovo na Serbia pamoja na Montenegro.

Wakati kama huo utamkuta Januzaj akicheza soka na ndugu zake wakiwemo binamu na baba zake wadogo. Lakini ndugu zake hao wanakumbuka maisha magumu waliyopitia wakati vita iliyosababishwa na ubaguzi wa kidini, kikabila baina ya Albania na Kosoro.

Mtoto mkubwa kati familia ya watoto sita, Abedin alikuwa akitegemewa na familia yake baada ya baba yake Idriz, mfanyakazi wa kiwanda cha nguo, kuanza kuumwa ugonjwa wa kansa. Lakini huku kukiwa na uwezekano wa kulazimishwa kujiunga na jeshi liliotawaliwa na waserbia la Yugoslav ili kupigana vita huko Bosnia, Abedin aliamua kuondoka kwenda Belgium mwaka 1992.

Wakati huo baba yake mdogo Abedin, Januz, tayari alikuwa kashafungwa kwa miaka 15 kwa kushiriki katika harakati za kuomba uhuru kutoka kwa Yugoslavia ambayo sasa ni Kosovo. Baadae mdogo wake, Shemsedin, alienda kujiunga na Januz katika jeshi la kupigania uhuru wa Albania.

Shemsedin, ambaye kwa sasa hana ajira yoyote akihangaika kwa hali na mali kuisadia familia yake ya mke na watoto wawili, anaeleza namna Abedin alivyokimbia ukandamizi wa Waserbia lakini kutafuta namna atakvyoweza kuisadia familia yao kwa kutuma fedha nyumbani. ‘Baba yangu alifariki miaka miwili baadae hivyo Abedin akawa ndio kichwa cha familia,' alisema.

Mke wa Abedin na mama yake Adnan, Ganimete Sadikaj, pia alikuwa mmoja ya wahanga wa ukandamizi. Alizaliwa kwenye moja ya familia za kitajiri huko Istog, familia ya Sadikajs ilikuwa inaonekana tishio na utawala wa Yugoslav baada ya vita vya pili vya dunia. Walilazimika kuondoka Kosovo na kwenda kuishi Uturuki.

Familia hiyo mwishoni ikahamia Belgium ambapo babu yake Adnan, Alija, alikuwa ameanzisha biashara zake huko na hatimaye mama na baba yake Adnan walipokutana na kuanzisha familia na matokeo ndio kinda hili linalotawala vyombo vya habari ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment