Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday, 20 October 2013

NIMEIJUA NA KUWA MPENZI WA SIMBA TANGU NIKIWA NA MIAKA SITA. NA NIMEWAFAHAMU YANGA TANGU WAKATI HUO.



Na msimu huu nimewaona Yanga na Simba wakicheza, tena na timu dhaifu kabisa, lakini, niweke wazi, kuwa kiwango cha soka kilichokuwa kikionyeshwa na Yanga ' B' na Simba ' B' enzi hizo ni cha juu zaidi kuliko Yanga na Simba ya leo.

Ni pale unapoangalia mechi ya Simba au Yanga halafu unaamua uchukue gazeti lililo mezani usome. Kwamba mchezo wa Simba au Yanga haumfanyi mtazamaji asahau kufanya mengine. Wanacheza soka iliyopooza.

Na leo itakuwa kama kawaida. Wenye kutanguliza ushabiki watataka kuona nani kashinda na nani kashindwa. Kisha washabiki waingie mitaani kutambiana.

Lakini, swali tunalopaswa kujiuliza ni je, Yanga na Simba wako kwenye viwango vya kuweza hata kushinda Ubingwa wa Afrika Mashariki?
Jibu langu limeshaeleweka, kuwa ni HAPANA!

Mechi ya leo itakuwa ya kupitisha siku na kutuongezea akiba ya maneno ya kutambiana mitaani, kama watani wa jadi.

Nikiweka pembeni mapenzi yangu kwa Simba ya tangu utotoni, Kimpira kwa sasa naifuatilia kwa karibu Mbeya City.

Hawa vijana ni hazina ya soka ya Tanzania. Wanacheza kandanda ya burudani na iliyojaa ufundi. Wanacheza wakifurahia soka.

Mbeya City ni Brazil ya Tanzania. Wakienda hivi hivi, naamini watachangia kwenye Mapinduzi ya Soka ya Tanzania.

Maggid Mjengwa.
Iringa.

No comments:

Post a Comment