Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 21 October 2013

ONAMASHABIKI WALIOZIMIA JANA KWENYE MATCH YA SIMBA NA YANGA,wengi ni wa Yanga yupo pia shabiki "MAMA YANGA"


Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) limesema watu 21 walianguka na kupoteza fahamu wakati wa mechi ya watani Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Watu walikuwa wakianguka mfululizo kila Yanga ilipofunga bao, likianza bao la Mrisho Ngassa. Baadaye mawili yaliyofungwa na Hamis Kiiza.

MAMA YANGA


Watu wa Red Cross walionekana kuchanganyikiwa kutokana na watu kuanguka mfululizo, wakati mwingine wakalazimika kuwabeba kwa mikono kutokana na vifaa kuwa vichache.
Mmoja ya walioanguka na kuzimia ni shabiki maarufu wa Yanga anayejulikana kama Mama Yanga.


Angukaanguka hiyo ilianza kuonekana upande wa Simba na hasa kipindi cha pili, mara tu baada ya timu hiyo kuanza kusawazisha.
Timu hizo zilimaliza mechi hiyo kwa sare ya mabao 3-3 wakati Yanga ikifunga mabao yake katika kipindi cha kwanza na Simba ikasawazisha yote katika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment