Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday 20 October 2013

Picha 5 za yule shabiki Steven wa Yanga alielia, akijiandaa kwenda kwenye mechi leo Picha 5 za yule shabiki Steven wa Yanga alielia, akijiandaa kwenda kwenye mechi leo


Ni shabiki mkubwa wa Yanga ambae alipata zaidi ya shilingi milioni 4 kwenye miezi miwili ya kwanza baada tu ya kuonekana kwenye TV akilia kwa uchungu kisa Yanga imefungwa tano, zikiwa ni pesa kutoka kwa watu mbalimbali ambao walimuonea huruma na wengine kujisikia tu kumpoozesha.

Ni muda umepita toka hiyo mechi ambapo leo tena Yanga na Simba kwenye uwanja wa taifa zinakutana ambapo Steven alipita mbele ya Camera ya millardayo.com na kuzungumza machache kuhusu hii mechi ya leo.

‘game ya leo ni nzuri japo maandalizi tumeshaanza muda mwingi sana tumejiandaa vizuri kwa hiyo tunategemea na sisi kupata ushindi sana, hatutegemei kama tutaipoteza hii game’ – Steven

Leo mkifungwa utalia tena? ‘leo nikifungwa ndio nitazimia moja kwa moja na kuna uwezekano nikaihama hata club kwa sababu imani yangu iko hapa tayari kwamba tutashinda ila tukifungwa tena nitaachia ngazi kistaarabu, nitamuandikia barua Muheshimiwa Manji manake yeye ndio alinipa cheti cha heshima cha uwanachama wa Yanga, kuhusu club gani nitahamia hiyo ni siri yangu’ -Steven

‘Yanga sasa hivi tuko kiprofeshino kama Barcelona sasa hivi au Real Madrid, Simba tutaiona manake imesajili sana mwaka huu kama kina Tambwe…. kwa hiyo tunategemea maushindi zaidi utakuepo, tena ushindi wa mawili kwa moja au moja bila… si hatuhitaji magoli matano, tunahitaji pointi tatu tu’ – Steven





No comments:

Post a Comment