
Ni mzazi ambae kazi yake kwa zaidi ya miaka 20 ni kuendesha Taxi jijini Dar es salaam kama unavyomuona kwenye picha akiwa na Taxi anayoimiliki, ni biashara ambayo ndio imemuwezesha kuwasomesha kina Madee na kuilea familia kwa miaka yote.
Anasema kwa miaka kadhaa hata mpaka sasa hivi, nyumbani kwake analea baadhi ya Wasanii ambao ni marafiki zake Madee, kwa sababu wanafanya muziki na Madee imebidi akubali hali halisi ya maisha ya mwanae ambapo toka miaka hiyo amewalea watu kama kina MB Dogg yani kama watoto wake, chakula kinapikwa pamoja wanakula na kulala kama familia.

Ni shabiki mkubwa wa Madee na anasikiliza sana nyimbo zake na hata kutokea kwenye video, faida mojawapo aliyoiona kutokana na muziki wa Madee, ni nyumba aliyowajengea kama Wazazi na nyumba nyingine Madee aliyoijenga kwa ajili ya kuishi yeye.

Tukio jingine analolikumbuka kuhusu Madee ni siku ambayo kundi la Ney wa Mitego lilikwenda nyumbani kwao huku likimkimbiza Madee spidi kwamba ni mwizi, Madee alipokimbilia nyumbani ndani ilibidi mama yake atoke kusawazisha na ndio ikawa siku ya mama yake kubaki na alama ya kudumu usoni baada ya mmoja kati ya waliokuwemo kwenye kundi la Ney wa Mitego kurusha chupa iliyompiga usoni.
Uhusiano kati ya Madee na Ney wa Mitego uko vizuri sasa hivi na wamekua marafiki na hata wakati mwingine Ney akitaka kutoa single ni lazima ammtumie Ney ili asikilize kwanza mfano ni wimbo wa ‘Salamu zao’ ambao unapata airtime kubwa kwenye radio sasa hivi.
No comments:
Post a Comment