Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 15 October 2013

WAJUE,Makipa wanaolipwa pesa ndefu Ulaya



SUPASTAA Mreno, Cristiano Ronaldo, ni mwanasoka anayelipwa fedha nyingi duniani kwa sasa. Staa huyo anapokea Pauni 15 milioni kwa mwaka baada ya makato ya kodi na kabla ya malipo ya bonasi nyingine.


Mashahara wake kwa wiki ni Pauni 288,000 akimwacha kwa mbali mwanasoka aliyesajiliwa kwa uhamisho ghali zaidi duniani kwa sasa, Gareth Bale ambaye analipwa Pauni 8.3 milioni kwa mwaka.


Lakini, mara nyingi imekuwa ikisikika juu ya wachezaji wa nafasi nyingine wakiongoza kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi na kulipwa mishahara mikubwa, lakini si makipa. Ushawahi kufikiria ni kipa gani analipwa fedha nyingi kwa sasa?


Makala hii inazungumzia makipa wanaolipwa fedha nyingi kwa mwaka katika klabu zao na kuweka rekodi. Achana na makipa kama Joe Hart, David De Gea, Pepe Reina, Hugo Iloris na Salvatore Sirigu, kuna makipa watano bora wanaovuta mshiko wa nguvu.


5. Victor Valdes - Barcelona


Kipa huyo Mhispaniola ambaye hivi karibuni alisema ataihama Barcelona mwishoni mwa msimu pale mkataba wake utakapofika tamati, ni miongoni mwa makipa wanaolipwa pesa nyingi katika klabu zao.


Valdes yumo kwenye tano bora. Kwa mwaka anavuta Pauni 5 milioni kutokana na mkataba wake wa sasa anaoutumikia Nou Camp.


4. Petr Cech - Chelsea


Ni mmoja wa makipa mahiri kabisa katika Ligi Kuu England kwa muongo uliopita. Kwenye klabu ya Chelsea, kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech analipwa Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.


3. Gianluigi Buffon - Juventus


Ni kipa aliyedumu kwenye kiwango bora kwa muda mrefu. Kwenye klabu ya Juventus, Buffon, anatazamwa kama nembo ya timu hiyo. Umahiri wake unamfanya kuwa kipa anayeingia mikataba minono inamfanya awemo kwenye orodha ya makipa wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwenye mchezo wa soka kwa sasa.


Buffon, ambaye kwa sasa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya Juventus ambayo ni bingwa wa Italia, analipwa Pauni 5.5 milioni kwa mwaka.
Ni miongoni mwa watu muhimu wanaoifanya Bayern Munich kuwa imara kwa sasa na kuendelea kutesa Ulaya ikiwa pamoja na msimu uliopita kunyakua mataji matatu; Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa kulipwa pesa nyingi baada ya kuvuta Pauni 5.6 milioni kwa mwaka katika huduma yake anayotoa Allianz Arena.
Lakini, Neuer alitarajia kuongeza mkataba mpya hivi karibuni ambao utamfanya kuwa na thamani kubwa zaidi.

1. Iker Casillas - Real Madrid
Mambo yake si shwari kwa sasa ndani ya Santiago Bernabeu kutokana na kusugua benchi. Kocha, Carlo Ancelotti, bado anamsubirisha kwenye benchi staa huyo wa Hispania, lakini jambo hilo halimfanyi kushindwa kuingiza pesa nyingi baada ya mabosi wa timu hiyo kumpatia mkataba mnono.
Mkataba wake ndani ya Real Madrid unamshuhudia Casillas akivuna Pauni 6.3 milioni kwa mwaka na kuwa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.
CHANZO MWANASPORT MTANDAONI.

No comments:

Post a Comment