Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 17 October 2013

KUMEKUCHA, Makocha wagwaya kutabirli Simba, Yanga

Dar es Salaam. Makocha wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara wamepatwa na kigugumizi kutabirlia matokeo ya mechi ya watani wa Simba na Yanga itakayopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi alisema amebahatika kuziona na kuzielezea kiufundi.

“Kwa bahati nzuri Simba na Yanga tayari tumecheza nao nimewaona ni wazuri wapi na udhaifu wao uko wapi. Kiufundi hazitofautiania sana. Simba ina wachezaji wa kigeni wanne kwenye kikosi chake cha kwanza sawa na Yanga, nafikiri viwango vyao vinalingana, hakuna tofauti kubwa.”

Nyota wa kigeni wa Yanga ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wakati Simba ina Abel Dhaira, Joseph Owino, Gilbert Kaze na Amis Tambwe.

“Tofauti nyingine ni kwamba kikosi cha Yanga kina wakongwe wengi wakati Simba yenyewe ina mseto wa vijana wengi ingawa haiwezi kuwa kipimo cha kushinda mchezo huo, nafikiri atakayetumia vizuri nafasi ndiye atakayeibuka mshindi,” alisema Mwambusi.


Naye Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime alisema: “Kiufundi, siwezi kusema lolote, kwa kuwa sifundishi moja kati ya timu hizo ingawa nafikiri hazitofautia. Siwezi kutabiri atafungwa nani ingawa atakaejipanga vizuri nafikiri ndiye atakayeshinda.”


Naye aliyekuwa Kocha wa Ashanti United, Hassan Banyai alisema: “Nafikiri timu zote mbili zinafungika na pia kwenye kufunga hazina matatizo, lolote linaweza kutokea, atakayemwahi mwenzake ndiye atayeshinda.”


Simba itaingia kwenye pambano hilo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-0 na Yanga kwenye mchezo uliopita yaliyopachikwa na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza.

No comments:

Post a Comment