Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 17 October 2013

ROONEY AOTA MAKUBWA BRAZIL


Mshambuliaji Wayne Rooney amesisitiza ameshukuru kuona England imefanikiwa kufuzu kwa Kombe la Dunia mwakani Brazil.
Rooney sasa amepata nafasi nyingine ya kuonyesha kipaji chake katika mashindano makubwa baada ya kufunga bao la kwanza na kuiongoza England kushinda 2-0 dhidi ya Poland kwenye uwanja wa Wembley.

Rooney anajua England ina nafasi ya kufanya makubwa Brazil kama akiendelea kucheza kwa kiwango cha juu hadi wakati huo.


“Hikchi ndichoo ninachotaka kufanya katika klila mashindano, lakini imekuwa haitokei nafasi,” alisema Rooney.
“Nataka kufanya vizuri na kuisaidia England kupata mafanikio. Sitaki kujiongezea presha mwenyewe, lakini ni wazi natakiwa kufanya vizuri zaidi. “

Unapocheza katika kikosi cha England ni wazi unatakiwa kuwa kushinda na kujaribu kutafuta mataji. “ Tuna wachezaji wengi vijana wenye viwango vya juu kama


Andros Townsend, Daniel Sturridge, Danny Welbeck, Jack Wilshere. Kama tutawatumia vizuri na kuwaongeza wazoefu naamini tutapata matokeo bora.


“Rooney amekuwa na mchango wa mkubwa kwa sasa baada ya kufunga mabao saba katika mechi sita za kufuzu na kumfanya kufikisha mabao 38 aliyofunga katika kikosi cha England.

No comments:

Post a Comment