Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 15 October 2013

MAJONZI, KOCHA ALIYEPELEKA SENEGAL ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA AFARIKI DUNIA KWA KANSA YA UTUMBO


Kocha wa zamani wa Senegal Bruno Metsu, ambaye aliiongoza nchi hiyo kufika robo fainali ya kombe la dunia mwaka 2002, amefariki dunia akiwa na miaka 59, vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti leo hii.

Gazeti la Local La Voix du Nord, sports daily L'Equipe na France Football magazine wameripoti kwamba Metsu, ambaye alistaafu kazi ya ukocha akiwa na klabu ya Al Wasl ya Dubai mwaka uliopita ili kupambana na kansa ya utumbo, alifariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Dunkirk kaskazini mwa France.

Metsu, ambaye alijulikana kama "The White Sorcerer", pia aliwahi kuifundisha Guinea, Qatar, na klabu kadhaa huko Uarabuni.

No comments:

Post a Comment