Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday, 18 October 2013

TANZANIA YAPOROMOKA VIWANGO FIFA




Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa) limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka kwa Oktoba, huku Tanzania ikiporomoka kwa nafasi mbili kutoka ile ya 128 hadi 130.
Licha ya kuporomoka, pia Tanzania imejikuta ikikamata mkia kwa ubora wa soka miongoni mwa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, Uganda imeteremka kwa nafasi nne kutoka 81 hadi 85, hata hivyo imeendelea kushikilia rekodi ya nchi inayoongoza kwa ubora kati ya nchi tano za Afrika Mashariki.

Nchi nyingine zinazounda jumuiya hiyo na viwango vyao vya ubora ni Ethiopia iliyoshuka kwa nafasi mbili kutoka 93 hadi 95, Kenya nafasi ya 118, wakati Burundi imepanda kwa nafasi mbili kutoka 120 hadi 122 na Rwanda ambayo pia imechupa kwa nafasi mbili kutoka 129 hadi 131.

Ivory Coast imeendelea kukaa kileleni ikishikilia nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka Afrika, huku ikipaa kwa nafasi mbili kutoka 19 hadi 17, wakati mabingwa wa Afrika, Nigeria wakiwa wamejitutumua na kupanda kwa nafasi tatu kutoka 36 hadi 33. Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment