Sunday, 22 December 2013
Bayern klabu bingwa ya dunia
Bayern Munich wamejiongezea taji jingine baada ya kuwafunga Raja Casablanca ya Morocco 2-0 na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia.
Katika mechi iliyopigwa jijini Marrakech kwenye falme ya Morocco, Wajerumani hao walijawa furaha kuongeza kombe hilo katika hazina yao
ambayo tayari ina makombe ya ubingwa wa Ulaya,
Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Uefa Super Cup.
Raja walikuwa wanajaribu kuwa klabu ya kwanza ya Afrika kutwaa taji hilo, lakini waliparaziwa mbali na Bayern wanaofundishwa na Pep Guardiola
kwa mabao ya Dante na Thiago Alcantara katika kipindi cha kwanza yalitosha kuwatangazia Bayern ufalme.
Hii ni rekodi kubwa kwa Guardiola, kwani katika kazi yake ya ukocha ametwaa kombe kama hili mara tatu, mara mbili za mwanzo akiwa na
Barcelona 2009 na 2011.
Bayern walipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi japokuwa Raja walikuwa na uungwaji mkono wa washabiki wa Morocco. Hata hivyo,
walichukuliwa kuwa timu dhaifu zaidi kwenye mashindano hayo lakini wakafanikiwa kuwafunga Auckland City, Monterrey na Atletico Mineiro ya
Ronaldinho.
Bayern kwa upande wao waliwafunga mabingwa wa Asia, Guangzhou Evergrande kutoka China.
Mabingwa wengine wa kombe hilo kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka jana ni Corinthians, Sao Paulo na Internacional zote za Brazil.
Wengine ni AC Milan (Italia), Manchester United (England), Barcelona (Hispania), Inter Milan (Italia), Barcelona (Hispania) na Corinthians wa
Brazil.
www.tabasamuleo.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment