Thursday, 26 December 2013
Katibu mpya TFF aingia na mikwara
Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa.
By Elius kambili,Mwananchi
KATIBU Mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, ameliambia Mwanaspoti kuwa jambo atakaloanza nalo akiingia ofisini ni kuziba mirija yote ya watu kujipatia fedha isivyo halali kupitia shirikisho hilo.
Muda mfupi baada ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi, kumtangaza Mwesigwa kushika wadhifa huo, Katibu huyo ameibuka akiliambia Mwanaspoti kwa kusema: “Unajua hii ni nafasi nyeti katika chombo kikubwa kama hiki ambacho kinaongoza soka la nchi nzima, mimi najipanga kuzuia mianya yote ya ulaji fedha ndani ya TFF, bila kufanya hivi naweza kushindwa katika kazi yangu.”
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 43 akiwa pia ni mtaalamu wa mambo ya sheria na uhusiano wa kimataifa, alisema jambo jingine atakalolifanyia kazi ni kuhakikisha weledi katika utendaji kazi unazingatiwa huku kila mfanyakazi akiwajibika katika nafasi yake.
Alisema atashirikiana vyema na watendaji wengine kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya muda mfupi na muda mrefu inatekelezwa kwa wakati katika muda wote wa kazi yake.
Mtendaji mwingine mpya wa TFF aliyetangazwa na Malinzi ni Evodius Mtawala ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Vyama, Wanachama na Masuala ya Kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment