Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 23 December 2013

HII NDIO TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS



Uongozi wa klabu ya Young Africans SC
umempatia taarifa (Notice) ya siku ya
thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie
Brandts juu ya kusitisha mkataba wake
kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa
matokeo mabaya katika michezo iliyopita
ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani
Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni
mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha
huduma na Brandts isichukuliwe kama
chuki bali ni moja ya sehemu ya
kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi
ili tuweze kupata matokeo mazuri katika
Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja
mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu,
na soka tulilocheza kwenye mchezo wa
mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri
mwalimu amefikia mwisho kimbinu na
hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini
ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali
iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na
wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30,
Brandts ataamua mwenyewe kama
ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au
kuondoka moja kwa moja kabla ya muda
huo ukiwa haujakamilika.
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu
itaendelea na mazoezi kama kawaida
katika kila siku asubuhi katika uwanja wa
bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya
kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred
Felix “Minziro”.
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom
na mashindano ya kimataifa uongozi
unakamilisha maandalizi ya safari ya
kambi nje ya nchi na taratibu zote
zitakapokamilika tutawajulisha.
Aidha uongozi upo katika mchakato wa
kumapata mrithi wa Brandts ambaye
ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi
ya mzunguko wa pili na Mashindano ya
klabu Bingwa Afrika.
Mwisho tunawaomba wanachama,
wapenzi na washabiki wa Yanga
wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya
bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi
unajipanga kuhakikisha timu inaimarika
kwenye benchi la ufundi na kurudisha
furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
www.hakileo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment