Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 24 December 2013

Simba wajazwa ‘manoti’

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umewazawadia wachezaji wake kitita cha Sh60 milioni baada ya kufanikiwa kuichapa Yanga mabao 3-1 katika pambano la Hisani lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akizungumza jijini jana, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Sued Nkwabi alisema, fedha hizo zimetolea kama njia moja wapo ya kuonyesha kuthamini juhudi zilizofanywa na wachezaji hao na kufanikiwa ushindi.Simba Sports Club

“Hakika ushindi tulioupata katika mechi dhidi ya Yanga umewapa raha Wanasimba wote ukizingatia kipindi tulichopo si kizuri sana nadhani kila mmoja anafahamu kinachoendelea Simba wakati huu,” alisema Nkwabi na kuongeza:


“Katika kuonyesha tunathamini juhudi zilizofanywa na wachezaji wetu kiasi cha kutupa ushindi mkubwa wa mabao 3-1 dhidi ya watani wetu Yanga uongozi umewazawadia wachezaji kiasi cha Sh60 milioni.”


Wakati huo huo,Nkwabi alisema kikosi cha Simba kitarejea Zanzibar, Desemba 29 tayari maandalizi ya Kombe la Mapinduzi litakaloanza kutimua vumbi visiwani humo kuanzia Januari Mosi hadi Januari 13 mwakani. “Wachezaji wetu kwa sasa watakuwa katika mapumziko ya sikukuu ya Krismasi lakini timu itarejea tena Zanzibar Desemba 29 kwa ajili ya kujiandaa na Michuano ya Kombe la Mapinduzi,” alisema Nkwabi na kuongeza:


“Tupo makini na michuano hii kwa vile lengo letu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa na ndiyo maana hata kocha wetu (Dzravko Lugarusic) atarejea nchini muda si mrefu kuendelea na progamu.”


Simba itafungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kuikabili AFC Leopards ya Kenya, Januari Mosi wakati mahasimu wao Yanga wenyewe wataivaa Tusker FC.

No comments:

Post a Comment