Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday, 23 December 2013

MANJI AWAOMBA WANACHAMA WA YANGA WASIVUNJIKE MOYO



Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.(P.T)


"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji.

Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.

Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

No comments:

Post a Comment