Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday 16 February 2014

NI MUHIMU YANGA KUYAFAHAMU HAYA KABLA YA KUMCHEZESHA OKWI.

Stori iliyoongoza kwa vichwa vya habari za michezo mwishoni mwa juma lililopita ilikuwa inamuhusu mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kilichopelea gumzo la mchezaji huyo ilikuwa ni baada ya FIFA kuiandikia barua TFF na kuitaarifu ya kwamba mchakato wa uhamisho wa Okwi toka SC Villa kwenda Yanga ulikuwa hauna tatizo. Lakini pamoja na kutoa taarifa hiyo FIFA bado ilisema yenyewe haina mamlaka ya kumruhusu mchezaji kuichezea klabu yake hiyo mpya zaidi ya kuiagiza TFF kufuatilia wenyewe taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo kama zipo sahihi.
Sasa hapo kwenye kufuatilia taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo ndipo kulileta utata,kutokana na angalizo hilo la FIFA iliulazimu mtandao huu kufuatilia kwa kina kuweza kujiridhisha na mahusiano yaliyopo hivi sasa kati ya Okwi na klabu ya Etoile Du Sahel iliyomnunua toka klabu ya Simba.

Baada ya kufanya mahojiano ya Raisi wa Etoile ndugu Ridha Charfeddinealiuhakikishia mtandao huu ya kwamba bado wana mkataba na mchezaji huyo ambao unakwisha mwezi june mwaka 2016.

Ni vizuri Yanga wakajiridhisha na haya kabla ya kumchezesha mchezaji husika.
Barua ya Etoile du Sahel waliyomwandikia Okwi wakimsihi arejee klabuni...
USAJILI
FIFA inasisitiza mchezaji kusajiliwa na timu moja tu ya soka kwa wakati mmoja, pia FIFA inasema wachezaji wanaruhusiwa kusajiliwa na klabu zisizozidi tatu kwa msimu mmoja. Kwa kipindi hicho mchezaji ataruhusiwa kuchezea timu zisizozidi mbili tu katika mechi rasmi. Kuna mwiko mmoja tu ambao unaruhusiwa kuvunjwa katika sheria hii, na huu ni pale ambapo mchezaji atakua amehama kati ya vilabu viwili ambavyo vinashiriki katika ligi zenye misimu inayofuatana.

Kwa mfano kama mchezaji kahama toka kwenye timu inayoshiriki ligi inayoisha katika mwezi wa tisa kwenda katika timu inayoshiriki ligi inayoanza mwezi wa kwanza, huyu ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu zake zote alizotoka na amezingatia sheria za usajili za chama cha soka cha nchi yake ikiwa ni pamoja na FIFA.

Maswali ya kujiuliza

1. Timu ipi kati ya Etoile na Yanga inammiliki mchezaji huyu wakati timu zote zimemsajili mpaka sasa wakati FIFA wanasisitiza mchezaji kusajiliwa na klabu moja tu kwa wakati mmoja,

2. kama FIFA wanasema mchezaji ataruhusiwa kuchezea timu nyingine ya pili katika ligi mpya aliyohamia ili mradi awe ametimiza masharti ya mkataba wake na timu zake zote alizotoka. Je Okwi ametimiza masharti na Etoile moja ya timu alizotoka ?

Kuvunja mkataba
Mkataba baina ya mchezaji wa kulipwa na klabu utaisha pale tu ambapo muda wa mkataba utafikia mwisho wake au mkataba kuvunjwa kwa makuballiano ya pande zote mbili lakini pia mkataba unaweza kuvunjwa na pande yoyote ile bila ya kuwa na vipingamizi ama adhabu pale tu ambapo kutakua na sababu ya muhimu inayotambulika kisheria.

Madhara ya kuvunja mkataba bila sababu maalum.

1. Mara zote upande unaovunja mkataba ndio unatakiwa kulipa gharama za uvunjaji mkataba.Gharama zinazohusika kulipwa ni zile zinazohusu mafunzo na kiwango huwa kinahesabiwa kutokana sheria za nchi,klabu na chama cha nchi husika.Gharama nyingine husika ni pamoja na madeni ya ada za uhamisho,mshahara wa mchezaji na marupurupu mengineyo.
2. Jukumu la ulipaji lazima libebwe na mchezaji ama akishirikiana na timu anayohamia.

3. Ushindwaji wa kulipa gharama hizi utasababishwa kutolewa kwa adhabu ya kufungiwa kucheza miezi minne ama miezi sita kutokana na uzito wa kosa. Adhabu hizi zitaanza kutumikiwa mara baada ya mchezaji husika kupewa taarifa rasmi. Adhabu hizi pia zitasimamishwa kuanzia mwisho wa msimu hadi mwanzo wa msimu mwingine ndipo zitakapoanza tena. Ingawa adhabu hizi huruhusiwa kuendelea kama mchezaji husika ni mmojawapo wa wachezaji katika timu ya taifa inayoshiriki fainali za mashindano yanayotambulika na FIFA.

4. Kwa ziada ya kulipa fidia baada ya kuvunja mkataba,adhabu za ziada zitatolewa kwa klabu ambayo itapatikana na hatia ya kutumia mbinu zisizo halali za kuchochea uvunjaji wa mkataba kabla ya kipindi kinachoruhusiwa. Klabu hiyo itafungiwa kusajili mchezaji yoyote kwa kipindi kisichopungua madirisha mawili ya usajili.
VIPENGELE MAALUM KUHUSU MIKATABA YA WACHEZAJI NA VILABU

Klabu nyingine yoyote yenye nia ya kuvunja mkataba wa mchezaji na klabu yake ya wakati huo italazimika kuifahamisha klabu ya mchezaji huyo kwa maandishi kabla ya kuanza mazungumzo na mchezaji. Mchezaji wa kulipwa ataruhusiwa tu kuanza mazungumzo na klabu nyingine ikiwa mkataba wake umeisha ama unatarajiwa kuisha ndani ya miezi sita.

No comments:

Post a Comment