BARCELONA imejiwekea mazingira mazuri ya kupenya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Manchester City, Uwanja wa Etihad usiku huu katika mchezo wa kwanza, hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Lionel Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 54 kwa penalti ya utata, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na Martin Demichelis, lakini refa akatenga tuta, kabla ya beki Dani Alves kufunga la pili dakika ya 90.
Mtu hatari; Messi akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa penalti usiku huu Uwanja wa Etihad
Hilo linakuwa bao la kwanza kabisa Messi anafunga dhidi ya vigogo wa Ligi Kuu ya England tangu ameanza kukutana navyo akiwa na Barca mwaka 2006 na kumaliza ukame wa kucheza saa 12 nchini humo bila kufunga.
Katika mchezo mwingine wa leo 16 Bora Ligi ya Mabingwa, Uwanja wa BayArena mjini Leverkusen, wenyeji Bayer 04 Leverkusen walichapwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain FC ya Ufaransa.
Mabao ya PSG yalifungwa Matuidi dakika ya tatu, pasi ya Verratti, Ibrahimovic dakika ya na 42 pasi ya Matuidi na Cabaye dakika ya 88 pasi ya Lucas.
Ndani ya eneo la hatari? Martin Demichelis akimkwatua Lionel Messi kusababisha penalti, lakini ilikuwa faulo ya ndani ya boksi? Na chini Messi akipiga penalti hiyo.
Shujaa: Ibrahimovic akishangilia baada ya kuifungia PSG
REKODI YA MESSI VIWANJA VYA LIGI KUU ENGLAND
2006: 16 Bora- Chelsea 1-2 Barca ilishinda
2006: Makundi– Chelsea 1-0 Barca ilifungwa
2007: 16 Bora – Liverpool 0-1 Barca ilishinda
2008: Robo Fainali – Man Utd 1-0 Barca ilifungwa
2009: Nusu Fainali – Chelsea 1-1 Barca ilitoa sare
2010: Kufuzu – Arsenal 2-2 Barca ilitoa sare
2011: 16 Bora – Arsenal 2-1 Barca ilifungwa
2012: Nusu Fainali – Chelsea 1-0 Barca ilifungwa
2014: 16 Bora – Man City 0-2 Barca ilishinda
No comments:
Post a Comment