Kiungo huyo kinda wa England alifunga bao la kwanza dakika ya 16 akimalizia pasi ya Lukas Podolski, aliyefunga bao la pili dakika ya 47.
Refa Howard Webb aliwapa penalti Liverpool baada ya Podolski kumchezea faulo Luis Suarez, na Steven Gerrard akaenda kufunga dakika ya 59.
Pamoja na hayo, Webb alimezea penalti nyingine ya Liverpool baada ya Oxlade-Chamberlain kumuangusha Suarez kwenye eneo la hatari.
Liverpool ilitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kusawazisha, lakini mwisho wa mchezo, Arsenal walifanikiwa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-1 Uwanja wa Anfield katika Ligi Kuu.

Kitu hicho: Alex Oxlade-Chamberlain akifunga bao la kwanza

Anashangilia

Luis Suarez akiwa haamini macho yake baada ya refa Howard Webb kuwanyima Liverpool penalti ya pili
No comments:
Post a Comment