Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 22 February 2014

JOHN TERRY AIBEBA CHELSEA ENGLAND

BAO la dakika ya mwisho kabisa la Nahodha aliyerejea John Terry limeipa Chelsea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton jioni hii katika Ligi Kuu ya England.
Ilikuwa kama Jose Mourinho tayari amekwishapoteza pointi mbili katika mbio za ubingwa kutokana na timu hizo kuwa hazijafungana hadi Phil Jagielka alipomchezea rafu Ramires.
Frank Lampard akaenda kupiga mpira wa adhabu ambao uliguswa na Branislav Ivanovic na Terry akateleza kwenda kuusukumia nyavuni dhidi ya kipa Tim Howard.
Baada ya ushindi huo wa mbinde unaoifanya Chelsea itimize pointi 60 baada ya mechi 27 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, na The Blues watasafiri hadi Galatasaray kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Hatua ya 16 Bora Jumatano.


Mkombozi: Frank Lampard (kushoto) na John Terry ushirikiano wao umeipa bao la ushindi Chelsea
John Terry alikuwa wa kwanza kuugusa mpira huku Slyvain Distin, Leighton Baines na Phil Jagielka wakiangalia
John Terry akiteleza kufunga dhidi ya Tim Howard

No comments:

Post a Comment