Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 22 February 2014

FLAMINI ALIVYOMTWANGA NGUMI WILSHERE BAADA YA KUZINGUANA MAZOEZINI JANA...NI SIKU CHACHE TU BADAA YA KUMPA MAKAVU OZIL

KIUNGO Jack Wilshere ameposti picha inayomuonyesha akipigana na mchezaji mwenzake Mathieu Flamini baada ya mazoezi jana kwenye basi la timu.
Viungo hao wawili walipigwa picha wakionekana kutofautiana kwenye mazoezi ya timu hiyo saa 24 kabla ya Arsenal kuwakaribisha Black Cats katika mchezo wa Ligi Kuu.

Wote utani: Wilshere ameposti picha hii inayomuonyesha akipigana na Mfaransa huyo kwenye basi la timu
+6

Nipishe: Jack Wilshere amehusishwa na kutofautiana na mchezaji mwenzake Mathieu Flamini kwenye mazoezi ya Arsenal jana na Bacary Sagna anaonekana kwenda kusuluhisha

Utaniambia nini: Wilshere akiongea kwa ishara ya mikono na Flamini huku Sagna akimfuata kumtuliza

Bacary Sagna alijitolea kutuliza hasira za wawili hao kwa kumsihi Wilshere atulie.
Lakini Wilshere akatweet kwa utani baadaye: "Flam hakufurahia wakati naondoka kwenye basi usiku! Samahani mwenzangu, naahidi kutotofautiana nawe tena!! #Hasira'
Sakata la wachezaji hao wawili wa Arsenal linakuja siku kadhaa baada ya Flamini kutaka kugombana hadharani na Mesut Ozil wakifungwa mabao 2-0 na Bayern Munich Uwanja wa Emirates
Kiungo huyo Mfaransa alimvaa Ozil akimtuhumu mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42.5 kutojituma kwenye mechi hiyo.
Arsenal wanarejea uwanjani leo kumenyana na Sunderland katika Ligi Kuu ya England wakitoka kutoa sare na Manchester United na kufungwa na Liverpool katika mechi zao mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment