Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 10 March 2014

RONALDO APIGA BONGE LA BAO REAL IKIUA 3-0 LA LIGA NA KUPAA KILELENI

MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameipaisha kileleni mwa LIga timu ya Real Madrid baada ya kufunga bao zuri la kichwa akiruka juu kama mcheza mpira wa kikapu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Levante usiku huu.

Ronaldo aliyefunga dakika ya 11 akiunganisha kona ya Angel Di Maria, pia alimsetia Marcelo kuifungia Real Madrid bao la pili dakika ya 49 na akamponza David Navarro kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Karabelas alifunga dakika ya 81 kuipa Real bao la tatu, hiyo ikiwa mechi ya 29 wanacheza bila kufungwa. Real sasa inatimiza pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 na kutulia kileleni, ikifuatiwa na Atletico Madrid pointi 64 baada ya mechi 27, wakati mabingwa watetezi, Barcelona ni ya tatu kwa pointi zake 63 baada ya kucheza mechi 27 pia.

Anatisha kijana: Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid dhidi ya Levante

+7
Amepaa juu: Cristiano Ronaldo akimruka kipa wa Levante, Keylor Navas

No comments:

Post a Comment