Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 10 March 2014

GOR MAHIA YAPIGWA 8-2 TUNISIA NA KUAGA LIGI YA MABINGWA, AFRIKA MASHARIKI HATUNA CHETU 16 BORA

Na Vincent Opiyo, Tunis
MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia wametolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 5-0 jana na wenyeji Esperance kwenye Uwanja wa Rades mjini Tunis katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza.
Matoeko hayo yanafanya Gor iage kwa kipigo cha jumla cha mabao 8-2 baada ya awali kufungwa mabao 3-2 nyumbani, Nairobi, Kenya.
Heithem Jouini alifunga mabao matatu dakika za 44, 48 na 56 na Harrison Afful na Idriss Mhrisi nao walifunga dakika za 54 na 74 kukamilisha ushindi mnono wa wenyeji.

Gor Mahia na Esperance katika mechi ya kwanza Nairobi. Picha kwa hisani ya Futaa.com

Mchezo huo ilikuwa ufanyike Jumapili, lakini ukasogezwa mbele kufuatia mvua kubwa mjini Tunis siku hiyo.Matokeo hayo yanamaanisha hakuna timu ya Afrika Mashariki iliyoingia Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo baada ya Yanga SC ya Tanzania kutolewa na Al Ahly ya Misri juzi kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
Kikosi cha Esperance kilikuwa; Ben Cherifia, Sameh Derbali, Khalil Chammam/Iheb Mbarki dk46, Chamseddine Dhaouadi, Ben Mansour, Khalid Mouelhi, Thiery Makon, Harisson Afful, Iheb Msakni/Idriss Mhrisi, Ahmed Akaichi na Heithem Jouini/Mohammed Ali Mhadhebi.
Gor Mahia; David Juma, Musa Mohammed/Oboya Patrick, Godfrey Walusimbi, Haron Shakava, David Owino, Antony Akumu, Geoffrey Kizito, Kevin Oluoch, George Odhiambo/Kevin Omondi, Timonah Wanyonyi/Rama Salim na Dan Sserunkuma.a

No comments:

Post a Comment